Pata taarifa kuu
SOMALIA-IS

Wanajihadi wa kundi la IS wauteka mji Qandala

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, Jumatano hii asubuhi Oktoba 25, wafuasi wa kundi la Islamic State walichukua udhibiti wa mji wa Qandala, mji wa ulio katika mkoa unaojitegemea wa Puntland. Ni kwa mara ya kwanza mji huu unaanguka mikononi mwa kundi la kijihadi nchini Somalia

mji wa Qandala mkoani Puntland umetekwa na kundi la Islamic State.
mji wa Qandala mkoani Puntland umetekwa na kundi la Islamic State. GOOGLE MAPS
Matangazo ya kibiashara

Huu hunda ukawa ushahidi tosha wa kusonga mbele kwa kundi la IS nchini Somalia. Kwa mujibu wa vyanzo rasmi, wanamgambo wa Kiislamu hamsini walishambulia mji huo Jumatano asubuhi. Baada ya mapigano ya muda mfupi na vikosi vya usalama, washambuliaji walichukua udhibiti wa mji huu wenye wakazi 20 000 unaopatikana kaskazini mashariki mwa mkoa unaojitegemea wa Puntland.

Kwa mujibu wa afisa wa Somalia aliyenukuliwa na shirika la habari la AFP, askari walikuwa wachache na walilazimika kuondoka katika mji huo. Afisa huyo amesema itakuwa ni mara ya kwanza kundi la Islamic State kudhibiti mji wa Somalia.

 

Pamoja na udhibiti wa mji huu, nguvu ya sasa ya kundi la Islamic state nchini Somalia bado ni vigumu kuitathmini. Kulingana na wataalamu idadi ya wapigananji wa kundi ili inatofautiana kati ya maelfu na mamia. Sehemu moja ni wawapiganaji wa kundi la Al Shabab waliojitenga na wengine. Mnamo mwezi Desemba 2015, jeshi la Kenya kwa mfano lilisema kuwa watu 200 wenye silaha walijiunga na kundi la IS.

Tangu kuibuka kwa kundi la Islamic, wapiganaji wa kundi la Al Shabab, ambao waliungana na kundi la al Qaeda tangu mwaka 2012, wamegawanyika kati ya wale wanaotaka kubaki katika kundi la al Qaeda na wale wanaojaribiwa na kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.