Pata taarifa kuu
DRC-UBELGIJI-USHIRIKIANO

DRC kuichukulia vikwazo Ubelgiji

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ina mpango wa kuichukulia 'vikwazo vikali' Ubelgiji katika kulipiza kisasi kwa uamuzi wa serikali ya Brussels wa kuzuia muda wa viza kwa viongozi wa DR Congo.

Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Februari 3, 2015.
Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Februari 3, 2015. © AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii iliyotangazwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Antoine Boyamba, inahusu kukataa kuwapa viza viongozi au raia wa Ubelgiji wanaomiliki pasi za kusafiria za kidiplomasia.

Wiki iliyopita, serikali ya Brussels ilitangaza kuzuia kwa kipindi cha miezi sita muda wa viza uliyokuwa umetolewa kwa watu au viongozi wa DR Congo wanaomiliki pasipoti za kidiplomasia.

Ubelgiji inatetea hatua hiyo ikibaini kwamba hali ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bado ni tete, na kuahirishwa hadi mwaka 2018 uchaguzi uliyokua umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ni sababu ya kucukuliwa hatau hii.

Hata hivyo Ubelgiji imeahidi kujadili katika siku zijazo mgogoro wa kisiasa nchini DRC na wafadhili wake wa Ulaya katika kikao cha Baraza la Ulaya.

Wiki hii serikali ya Kinshasa ilimtuma mjini Brussels waziri wake wa Viwanda, Kambinga Germain, baada ya viongozi wa Ubelgiji kutangaza vikwazo juu ya visa kwa viongozi wa DR Congo.

"Napenda nijuwe ni uhusiano upi ulio kati ya viza zinazotolewa kwa viongozi na hali ya kisiasa nchini DR Congo," Bw Kambinga amesema katika mahojiano na BBC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.