Marekani yaamuru familia za wafanyakazi wake kuondoka DR Congo
Serikali ya Marekani inataka Familia za wafanyikazi wake wanaofanya kazi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuondoka nchini humo haraka iwezekanavyo, kwa sababu za kiusalama.
Imechapishwa:
Marekani inasema inahofia kuwa huenda kukatokea machafuko katika jiji kuu la Kinshasa na miji mingine, kutokana na harakati za kisiasa kama ilivyokuwa wiki iliyopita.
Hatua hii inakuja baada ya Marekani kuwawekea vikwazo washirika wawili wa rais Joseph Kabila kutokana na machafuko yaliyotokea hivi karibuni na kusababisha maafa, kumshinikiza rais wa nchi hiyo kuendelea kuwa madarakani wakati muda wake utakapofika mwisho.
Msemaji wa Serikali ya DRC Lambert Mende, ameishtumu hatua hiyo ya Marekani, na kudai inapanga kuleta machafuko nchini mwake.