Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-UFARANSA

Raia wawili wa Ufaransa wauawa kikatili nchini Madagascar

Polisi nchini Madagascar wanachunguza mauaji ya watu wawili raia wa Ufaransa, waliokuwa wakifanya kazi za kujitolea nchini humo, ambapo watu wawili tayari wamekamatwa kuhusiana na

Moja ya fukwe ya bahari iliyopo kwenye kisiwa maarufu cha Sainte Marie nchini Madagascar, ambako raia wa Ufaransa waliuawa.
Moja ya fukwe ya bahari iliyopo kwenye kisiwa maarufu cha Sainte Marie nchini Madagascar, ambako raia wa Ufaransa waliuawa. DR
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini Madagascar zinasema kuwa watu wa nne wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo, ambapo wanadaiwa kuwa walikuwepo kwenye klabu moja ya usiku ambapo raia hao wawili wa Ufaransa walikuwepo siku ya Jumapili, lakini bado hawajabaini sababu za kutekelezwa kwa mauaji hayo.

Polisi wanasema kuwa, hakuna ubishi kuwa wafanyakazi hao wa Ufaransa waliuawa, na kwamba wanachokifanya sasa ni kubaini sababu za kutekelezwa kwa mauaji hayo.

Miili ya raia hao wawili wa Ufaransa, ilipatikana katika fukwe ya bahari ya hoteli moja ya kitalii kwenye pwani ya Madagascar, wakiwa na majeraha ya kichwani.

Raia hao wanaelezwa kuwa walikuwa wakijitolea kwenye shirika moja la Cetamada linalojihusisha na masuala ya mazingira na hasa ulinzi wa maliasili za bahari.

Kwa mujibu wa mamlaka kwenye mji wa Sainte Marie, kisiwa ambacho ni maarufu kwa utalii, wanasema kuwa, hii ni mara ya kwanza kwa raia wa Ufaransa kuuawa.

Mwaka 2012 wanandoa wawili wa Ufaransa, pia walipatakina wameuawa kwenye fukwe moja kusini mwa nchi ya Madagascar.

Mwaka mmoja baadae, raia wawili wa Ulaya walishambuliwa na kuuawa na kundi la watu kaskazini mwa kisiwa cha Nosy Be, wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya kijana mmoja mzaliwa wa Madagascar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.