Pata taarifa kuu
RWANDA-AU

Viongozi wa Afrika washindwa kumchagua Mwenyekiti mpya wa Tume ya AU

Viongozi wa mataifa ya Afrika wameshindwa kumchagua Mwenyekiti mpya wa Tume ya Umoja huo katika mkutano ya viongozi hao jijini Kigali nchini Rwanda.

Mkutano Mkuu wa viongozi wa Afrika jijini Kigali nchini Rwanda
Mkutano Mkuu wa viongozi wa Afrika jijini Kigali nchini Rwanda cebook.com/AfricanUnionCommission
Matangazo ya kibiashara

Hii inamaana kuwa Mwenyekiti wa sasa Nkosazana Dlamini-Zuma ambaye alikuwa ametangaza kutowania tena wadhifa huo ataendelea kuongoza hadi mwezi Januari mwaka ujao wakati uchaguzi mwingine utakapofanyika.

Msemaji wa Dlamini Zuma, Jacob Enoh Eben kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema baada ya mzunguko wa kwanza wa upigaji kura na kubainika kuwa hakuna mgombea aliyepata theluthi mbili ya kura ili kupata mshindi huku mataifa 28 kati ya 54 yakisusia zoezi hilo la kupiga kura.

Kulikuwa na wagombea watatu, aliyekuwa Makamu wa rais wa Uganda Specioza Wandira Kazibwe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje wa Bostwana Pelonomi Venson-Moitoi na Agapito Mba Mokuy ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani wa Mambo ya nje ya Equatorial Guinea.

Wiki iliyopita, kulikuwa na wasiwasi ikiwa uchaguzi huu ungekuwepo wakati wa kikao hiki cha 27 kwa madai kuwa hapakuwa na mgombea sahihi wa kuchukua nafasi ya Bi.Zuma kutokana na ushawishi wa mataifa yenye uchumi mkubwa barani Afrika kama Nigeria na Afrika Kusini.

Majukumu makubwa ya Mwenyekiti mpya itakuwa ni kushughulikia maswala ya amani, usalama na siasa barani Afrika, biashara na viwanda, miundo mbinu, maswala ya kijamii na Sayansi na teknolojia.

Dlamini Zuma kutoka Afrika Kusini alichaguliwa katika nafasi hiyo mwaka 2012 na kuchukua nafasi ya Jean Ping kutoka Gabon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.