Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-SALVA KIIR-RIEK MACHAR

Rais Salva Kiir aamuru kusitishwa haraka kwa mapigano

Nchini Sudan Kusini, Rais Salva Kiir amesaini sheria inayoamuru "usitishwaji wa uhasama haraka iwezekanavyo kuanzia saa12h00 jioni saa za Sudan Kusini (sawa na saa 9:00 saa za kimataifa), kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa katika televisheni na Waziri wa Habari, Michael Makuei.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, azitaka pande zinazohasimiana kuweka silaha chini.
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, azitaka pande zinazohasimiana kuweka silaha chini. Reuters/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Mapigano kati ya majeshi ya ya serikali na waasi wa zamani yalianza upya katika mji mkuu, Juba, siku tatu zilizopita.

Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa Jumatatu hii katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, kati ya vikosi vinavyomtii Rais Salva Kiir na vile vinavyomuunga mkono Makamu wa kwanza wa rais Riek Machar.

Ndege za kivita na vifaru vimeonekana vikitumiwa katika mapigano hayo. Hali hii imesababisha usalama kudorora katika taifa hili changa duniani, na kutishia kuzuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mapema Humatatu asubuhi Serikali ya Marekani, imetaka kusitishwa mara moja kwa vurugu nchini Sudan Kusini, baada ya kutokea mapigano mapya, jijini Juba, mapigano yanayotishia kuvunjika kwa mkataba wa amani kwenye taifa hilo jipya kabisa duniani.
 Mapigano haya ni ya kwanza kati ya jeshi la Serikali na wanajeshi waasi mjini Juba, toka kurejea nyumbani kwa kiongozi wao, Riek Machar mwezi April mwaka huu, na kuchukua nafasi ya makamu wa kwanza wa Rais, kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu nchini humo kwa miaka 3.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, imeagiza kuondoka nchini humo kwa raia na wafanyakazi wake, na kulaani taarifa kuwa raia wa kawaida wemeshambuliwa, ambapo mpaka sasa watu 150 wamekufa kutoka kila upande.

"Natoa wito kwa utulivu na kujizuia katika mapigano hayo. Mimi niko salama Hakuna anayeweza kutumia haki yake kwa kuhatarisha usalama wa nchi, " Riek Machar ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.