Pata taarifa kuu
LIBERIA-UNMIL-JOHNSON SIRLEAF

Liberia yachukua udhibiti wa usalama wake wa ndani

Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia (UNMIL) itakabidhi majukumu yake kwa serikali ya Liberia, Alhamisi hii Juni 30. Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia, iliyoundwa mwaka 2003, baada ya miaka 14 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mpaka sasa ilikua na askari 15,000.

Rais wa Liberia Ellen Johnson-Sirleaf, Mei 17, 2013.
Rais wa Liberia Ellen Johnson-Sirleaf, Mei 17, 2013. Reuters/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Ilisaidia utulivu, amani na usalama kurejea nchini humo. Kwa hiyo Mamlaka ya Liberia inakabidhiwa Alhamisi hii majukumu ya kudhibiti usalama wake wa ndani. Lakini zoezi hili la kukabidhiana majukumu hayo, wengi wanaona kwamba huenda likaleta changamoto na athari.

Kutoa ulinzi katika viwanja vya ndege, fedha kutoka nje, kukagua silaha au kufanya doria katika bahari, yote hayo yamekua yakisimamiwa na tume ya Umoja wa Mataifa nchini Liberia, na yatakabidhiwa serikali ya nchi hiyo. Majukumu hayo yatasimamiwa na askari polisi 5 000 na wanajeshi 2 000 kutoka Liberia.

Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, anasema kuwa na imani kwamba kazi hiyo itaendeshwa kwa ujasiri. Kwa mujibu wa rais wa Liberia, nchi yake inapaswa kuonyesha ulimwengu kwamba sasa imekua na inaweza kudhibiti usalama wake. Hata hivyo, uwezo wa kifedha kuna hatari ukosekane. Bajeti ya usalama wa Liberia inafikia dola milioni 90. Kiwango kilio chini mara tatu kwa kile cha UNMIL.

Hatima gani kwa maveterani?

Hatima ya maveterani inaibua maswali maswali mengi. Wanamgambo wengi wa zamani wamebaki ni hafifu na hawana kazi. Wanakabiliwa hasa na matatizo ya kisaikolojia na ulevi.

Changamoto nyingine ni kuingiza siasa katika vikosi vya usalama. Kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la Joint Action Commitee, kuna hatari ya mgogoro mkubwa. Kundi hili la wapinzani linamtuhumu Rais Sirleaf kutaka kutumia jeshi na polisi kukandamiza wapinzani wake kabla ya uchaguzi wa urais wa 2017.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.