Pata taarifa kuu
NIGERIA

Mawaziri zaidi wapandishwa kizimbani Nigeria

Mawaziri wawili waliokuwa kwenye Serikali ya rais Goodluck Jonathan nchini Nigeira, wameshtakiwa kwa wizi wa dola za Marekani milioni 17 kupitia mifuko ya Serikali na utakatishaji fedha, imesema taarifa ya kitengo cha kupambana na fedha haramu.

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ambaye toka ameingia madarakani ameendelea kukabiliana na mawaziri wala rishwa hasa waliokuwa kwenye utawala uliopita
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari ambaye toka ameingia madarakani ameendelea kukabiliana na mawaziri wala rishwa hasa waliokuwa kwenye utawala uliopita REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri hao, Nenadi Usman na Femi Fani-Kayode ambao walihudumu kwa nyakati tofauti kama waziri wa fedha na mwingine waziri wa masuala ya anga ndani ya chama cha PDP kilichokuwa cha rais Olusegun Obasanjo, ambaye muhula waka ulitamatika mwaka 2007.

Mawaziri hao wa zamani ambao walipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza juma hili kwenye mahakama kuu ya jijini Lagos, baada ya kusomea mashtaka, walikana kuhusika na wizi huo.

Usman alikuwa mkuu wa kitengo cha fedha ndani ya chama tawala cha PDP wakati wa kampeni za urais huku mwenzake Kayode alikuwa mkuu wa kitengo cha matangazo wa chama kwenye kampeni zilizoshuhudia chama hicho kikianguka.

Kitengo cha kupambana na fedha haramu kinasema watuhumiwa wote wawili waliiba na kinyume cha sheria walitumia Naira bilioni 4.9 zilizokuwa fedha za uma kwa masuala ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.