Pata taarifa kuu
NIGER-HAMA-SIASA-SHERIA

Niger: mgombea Hama Amadou aachiliwa huru kwa muda

Mahakama ya Rufaa ya mjini Niamey Jumanne hii Machi 29, imemuachilia huru kwa muda mgombea wa upinzani Hama Amadou, ambaye analazwa hospitalini nchini Ufaransa tangu Machi 16 baada ya kusafirishwa kutoka jela alikokua akizuiliwa nchini Niger.

Kiongozi mkuu wa upinzani Niger, Hama Amadou, Novemba 16, 2013.
Kiongozi mkuu wa upinzani Niger, Hama Amadou, Novemba 16, 2013. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Hama Amadou aliwekwa jela kwa tuhuma ya biashara ya watoto. Taarifa hii ya kuachiliwa huru kwa muda kwa kiongozi huyo mkuu wa upinzani nchini Niger imetolewa na mmoja wa wanasheria wake.

"Uamuzi uko wazi: Mahakama (ya Rufaa) imeagiza kuachiliwa huru kwa muda mgombea Hama Amadou. Yuko huru kuanzia leo" amesema mbele ya vyombo vya habari, Mossi Boubacar, mmoja wa wanasheria wa Hama Amadou, ambaye alikua jela kipindi chote cha kampeni za uchaguzi wa rais.

Baada yakuruhusiwa kuondoka hospitalini mjini Paris ambapo anafanyiwa huduma za kimatibabu, Bw Amadou hatourudi gerezani mjini Filingué, kilomita 180 kaskazini mwa mji wa Niamey, kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na kesi hiyo.

"Bw Amadou anaweza kuruhusiwa kuondoka hospitalini leo au kesho" daktari wake kutoka mji wa Paris, Luc Karsenty, wa hospital Marekani mjini Paris,ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP. Hama Amadou ataendelea kuhudumiwa hadi atakapopata nafuu akiwa mjini Paris kwa muda wa mwezi mmoja," daktari ameongeza.

Hama Amadou anatuhumiwa kufanya biashara ya watoto, kesi ambayo inachafua hali ya siasa nchini Niger kwa miaka miwili sasa na ambapo watu ishirini wamehusishwa. Hama Amadou ameendelea kuthibitisha kwamba ni mpango wa kumchafua na kumuangusha kisiasa ili asiwezi kugombea kwenye kiti cha urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.