Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-ETOILE DU SUD-MAUAJI

Grand-Bassam: raia 15 na askari polisi 3 wameuawa

Raia 15 na askari polisi 3 wa vikosi vya usalama ndio waliuuawa Jumapili hii katika mashambulizi ya kijihadi dhidi ya mji wa kitalii wa Grand-Bassam, karibu na mji wa Abidjan, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cote d'Ivoire, Hamed Bakayoko, ametangaza Jumatatu hii. 

Askari polisi wakiendesha uchunguzi wao mbele ya hoteli ya Etoile du Sud, katika mji wa Grand Bassam, Cote d'Ivoire, Machi 14, 2016, siku moja Baada ya shambulizi la kigaidi.
Askari polisi wakiendesha uchunguzi wao mbele ya hoteli ya Etoile du Sud, katika mji wa Grand Bassam, Cote d'Ivoire, Machi 14, 2016, siku moja Baada ya shambulizi la kigaidi. ISSOUF SANOGO/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Magaidi watatu waliuawa," Bw Bakayoko ameongeza katika mkutano na waandishi wa habari baada ya kikao kisichokua cha kawaida cha baraza la mawaziri, tofauti na takwimu rasmi ziliotangazwa na serikali Jumapili jioni ambapo Rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara alisema kwamba raia 14 na askari wawili wa vikosi vya usalama waliuawa. Upande wa washambuliaji, sita waliuawa na vikosi vya usalama.

Katika taarifa yake iliorushwa hewani Jumapili usiku, kundi la AQMi lenye mafungamano na Al-Qaeda lilisema kuwa watu walioendesha shambulio hilo walikua watatu.

Kwa mujibu wa chanzo cha serikali, vikosi vya kwanza vya usalama waliwafananisha wahanga na wauaji.

Kwa upande mwingine, askari wa vikosi maalum aliejeruhiwa wakati wa mapambano dhidi ya wapiganaji wa kijihadi alifariki usiku wa kuamkia Jumatatu hii, chanzo hicho kilmesema.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Cote d'Ivoire amesema watu 33 walijeruhiwa, ikiwa ni pamoja na 26 ambao bado wamelazwa hospitalini.

Waziri Bakayoko Ameahidi kutoa maelezo zaidi juu ya utambulisho wa wahanga sawa na washambuliaji mara tu mwendesha atamaliza "zoezi kamili la kutambulisho".

Aidha, Bw Bakayoko, akizungumza kwa niaba ya serikali, amebaini kwamba siku tatu za maombolezo zimetangazwa na amesisitiza kuwa usalama utaimarishwa katika "maeneo muhimu na katika kunakokusanyika watu wengi (... ) shule, balozi, ofisi za mashirika mbalimbali ya kimataifa, makazi ya wanadiplomasia (...) na mipakani. "

"Lengo la (wanajihadi) ni kutia uoga. Jibu la kwanza ni kutokua na hofu. Sisi raia wa Cote d'Ivoire tutasimama kidete," amesema Bw Bakayoko, huku akiongeza kuwa "Cote d'Ivoire haitoacha kusonga mbele."

Raia 4 wa Ufaransa waliuawa katika shambulio la Grand-Bassam

Kwa upande mwengine, Ikulu ya Ufaransa imeongeza Jumatatu hii idadi ya raia wa Ufaransa waliouawa katika shambulio lililotokea katika hoteli ya Etoile du Sud katika mji wa kitalii wa Grand-Bassam. “Idadi imeongezeka, kwani raia wanne wa Ufaransa hatimaye waliuawa katika shambulio la Grand-Bassam. Rais wa Jamhuri anatoa rambirambi zake kwa familia za wahanga”, imebaini taarifa ya Ikulu ya Ufaransa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.