Pata taarifa kuu
RWANDA-ICTR

Mauaji ya kimbari: ICTR yafunga milango yake

Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda ICTR iliyoanzishwa mwaka 1994 baada ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda inamalizia rasmi kazi yake Alhamisi hii, Desemba 31.

Ofisi ya Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda mjini Arusha.
Ofisi ya Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda mjini Arusha. © (CC)/Tomsudani/Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Hukumu ya watuhumiwa wa mauaji ya kimbari yaliotokea nchini humo itaendelea: ICTR imetuma kesi kadhaa kwa taasisi inayohusika na Utaratibu kwa Mahakama za Kimataifa za Uhalifu, ambazo zitafuatilia kesi hizo. Na kisha mahakama za kitaifa inaweza kuchukua hadi kesi.

Wakati huo huo raia wa Rwanda aliyekua akiishi nchini Ujerumani tangu mwaka 2002 alihukumiwa Jumanne wiki hii na mahakama ya Frankfurt kifungo cha maisha kwa kuhusika kwake katika mauaji ya kimbari.

Katika muda wa miaka 20 ya kazi, Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda imewafungulia mashtaka watu 93: 61 walikutwa na hatia, 14 waliachiwa huru.

Hatimaye, wanane kati ya watuhumiwa hao 93 bado hawajakamatwa, ikiwa ni pamoja na mfanyabiasha mashuhuri Félicien Kabuga, anayedaiwa kuwa mfadhili mkuu wa mauaji ya kimbari.

Viongozi wa nagazi za juu

Nembo  ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda, ICTR.
Nembo ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda, ICTR. Wikimedia

Hukumu iliyotolewa hivi karibuni na ICTR ni ile ya Desemba 14 katika kesi dhidi ya Waziri wa Maendeleo ya anawake, Pauline Nyiramasuhuko, pamoja na washitakiwa watano wenzanke. Ni mwanamke wa kwanza kushtakiwa kwa mauaji ya kimbari na mahakama ya kimataifa.

Katika majukumu yake, ICTR kimsingi ingelipaswa kuwahukumu watuhumiwa wa ngazi ya juu, wale ambao walihusika kwa kiasi kikubwa katika mauaji ya kimbari. Mahakama hiyo iliwahukumu viongozi maarufu kama Waziri mkuu wa zamani Jean Kambanda, mkuu wa zamani wa jeshi, Jenerali Augustin Bizimungu na mkurugenzi wa zamani wa wizara ya Ulinzi, Kanali Theoneste Bagosora.

Mahakama za kitaifa

Mahakama za kitaifa, kama vile Ufaransa, Ubelgiji, Finland zinaweza kusikiliza kesi ambazo zilikua bado hazijashughulikiwa na ICTR. Miongoni mwa washitakiwa 93, ICTR iliwatuma watuhumiwa kumi katika mahakama za kitaifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.