Pata taarifa kuu
Tanzania-Nyerere Day

Miaka 16 tangu kutokea kwa kifo cha Nyerere

Hii leo watanzania wameadhimisha kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa taifa Mwalim Julia Kambarage Nyerere aliefariki dunia katika hospitali ya mtakatifu Thomas jini London nchini Uingereza.

baba wa taifa nchini Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
baba wa taifa nchini Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Matangazo ya kibiashara

Mwalim Julius kambarage Nyerere alizaliwa April 13 mwaka 1922 huko Butiama Mkoa wa Mara, na kufariki tarehe kama ya leo Octoba 14 mwaka 1999. alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania. Nyerere alikuwa mwenyekiti wa Tanu na baadae CCM.

Mwalim Nyerere aliingoza tanzania tangu mwaka 1961 hadi mwaka 1985, na kalba ya kuingia kwenye siasa alikuwa Mwalimu Kazi hii ndiyo ilimpatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu." Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiyari baada ya kutawala kwa muda mrefu.

Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

Mbali na hayo Hayati nyerere aliwaasa sana viongozi wa Tanzania kuhusu swala la kupiga vita rushwa, ambalo limekuwa changamoto kubwa.

mbali na kukumbukwa na watanzania, mwalim Nyerere anakumbukwa pia na waafrika kote barani hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika. Ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.