Pata taarifa kuu
BURKINA-USALAMA-SIASA

Burkina Faso: Waziri wa mpito Isaac Zida ameachiliwa huru.

Waziri Mkuu wa mpito nchini Burkina Faso, Isaac Zida, amekua akishikiliwa na wanajeshi waliofanya mapinduzi tangu Jumatano wiki iliyopita. Isaac Zida ameachiliwa huru Jumanne hii asubuhi.

Waziri Mkuu wa mpito wa Burkina Faso Isaac Zida achukuliwa kama adui na wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais.
Waziri Mkuu wa mpito wa Burkina Faso Isaac Zida achukuliwa kama adui na wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais. AFP PHOTO
Matangazo ya kibiashara

Isaac Zida ameondoka katika Ikulu ya Rais na amejielekeza rasmi nyumbani kwake. Spika wa bunge la Mpito, Cherif Sy amekutana naye.

Cherif Sy amehakikisha kwenye RFI kwamba Waziri Mkuu anaendelea vizuri, na ametafsiri kuachiliwa huru kwake kama ishara ya amani kwa upande wa wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa wa Rais (RSP).

Hayo yakijiri jeshi la Burkina Faso limeingia katika mji mkuu wa nchi hiyo, Ouagadougou, usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne wiki hii, ambapo linajadili kujisalimisha kwa wanajeshi wa kikosi cha ulinzi cha Rais ambao waliipindua serikali Jumatano wiki iliyopita.

Wakati huo huo Rais Michel Kafando ambaye alikua akizuiliwa na viongozi kadhaa katika serikali yake ameachiliwa huru

“ Wanajeshi wote wa Burkina Faso (waliohamasishwa Jumatatu wiki hii kuelekea katika mji mkuu), wameingia Ouagadougou usiku wa kuamkia leo Jumanne ”, kanali Serge Alain Ouédraogo, naibu mkuu wa vikosi vya usalama ameliambia shirika la habari la Ufaransa la AFP.

“ Tunataka wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais waliofanya mapinduzi ya serikali Septemba 17 wajisalimishe, bila kumwagika damu ”, ameongeza kanali Serge Alain Ouédraogo.

Vikosi vya jeshi kutoka mikoa mbalimbali nchini Burkina Faso wameingia Jumatatu jioni katika maeneo yalio karibu na mji mkuu, ambapo sheria ya kutotoka nje usiku imewekwa tangu Alhamisi wiki iliyopita. wanajeshi hao walisitisha msafara wao Jumatatu jioni wakiwa karibu na mji mkuu ili kujadili kujisalimisha kwa wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais waliohusika na mapinduzi ya serikali.

Wakuu wa jeshi walitoa agizo Jumatatu alaasiri kwa wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa Rais " kuweka chini silaha " na kuonya kuwa majeshi yako njiani kuelekea katika mji mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.