Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-AJALI-USALAMA

Sudan Kusini: zaidi ya watu 200 wamefariki katika mlipuko wa lori la mafuta

Mlipuko uliosababishwa na ajali ya lori lililokua ikibeba petroli umewaua zaidi ya watu 200 mamia wengine wamejeruhiwa nchini Sudan Kusini. Ajali hiyo ilitokea Jumatano Septemba 16 katika mkoa wa magharibi mwa mji mkuu wa Juba.

Mwaka 2010, mlipuko wa lori la mafuta uligharimu maisha ya zaidi ya watu 230 na mamia waliojeruhiwa nchini  RDC.
Mwaka 2010, mlipuko wa lori la mafuta uligharimu maisha ya zaidi ya watu 230 na mamia waliojeruhiwa nchini RDC. RFI / Sébastien Nemeth
Matangazo ya kibiashara

Mkoa huo unakabiliwa na ukosefu wa vifaa vya matibabu ili kuwahudumia watu waliopata mareruhi kutokana na moto.

Mlipuko wa lori la petroli umewauawa zaidi ya watu 200 nchini Sudan Kusini. Gari iliyokuwa imejaa mafuta ilikua kwenye barabara inayoonganisha Juba na Maridi, kwenye umbali wa kilomita 300 magharibi mwa mji mkuu.

Awali serikali ilitangaza watu 85 kuwa ndio waliuawa na mlipuko huo.

Lori hilo la mafuta, lililokua limefanya ajali, hatimaye lilipuka. Msemaji wa Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ndiye alitoa maelezo ya ajali hiyo iliyotokea Jumatano, Septemba 16. Zaidi ya watu 100 pia walijeruhiwa. Watu hao wanasumbuliwa na majeraha kutoka na kuungua kwa moto, baada ya lori lililokua likisheheni mafuta kulipuka, amesema afisa huyo.

Watu hao wamefariki wakijaribu kuokoa mzigo wa mafuta katika makopo, tukio ambalo hutokea mara kwa mara katika ukanda huo kunakotokea uvujaji wa mabomba ya mafuta kwenye malori, au ajali la malori ya mafuta. Mwezi Juni mwaka 2013, watu 30 ambao walikuwa wakijaribu kuokoa mafuta kutoka lori moja lililokua na tatizo waliuawa nchini Uganda. Mwezi Julai mwaka 2010, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), watu 230 walifariki katika mlipuko wa ajali lori la mafuta. Mwezi Desemba mwak 2006, watu 284 walifariki nchini Nigeria katika mlipuko wa bomba la mafuta mjini Lagos.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.