Pata taarifa kuu
BURKINA-USALAMA-SIASA

Jumuiya ya kimataifa yaomba Kafando na Zida waachiliwe huru

Rais wa Burukina Faso Michel Kafando na Waziri Mkuu Isaac Zida na mawaziri kadhaa wanaendelea kushikiliwa katika Ikulu ya wa rais mjini Ouagadougou na watu wenye silaha.

Waandamanaji katika mji wa Ouagadougou karibu na Ikulu ya Rais, Septemba 16.
Waandamanaji katika mji wa Ouagadougou karibu na Ikulu ya Rais, Septemba 16. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya kimataifa imetoa wito wa kuachiliwa huru kwa viongozi hao mbalimbali kwa minajili ya kuendeleza mchakato wa mpito nchini humo. Umoja wa Afrika, ECOWAS na Umoja wa Mataifa walitoa tamko la pamoja, wakilaani kitendo hicho.

Wakati ambapo Rais wa Burkina Faso Michel Kafando na Waziri Mkuu Isaac Zida wakiendelea kuzuiliwa, baada ya kushikiliwa na watu wenye silaha tangu Jumatano jioni wiki hii katika Ikulu ya rais, hisia tofauti zimeanza kutolewa katika jumuiya ya kimataifa. Umoja wa Afrika, ECOWAS na Umoja wa Mataifa wametoa Jumatano jioni tanagazo la pamoja kwa vyombo vya habari. Taasisi hizo zimebaini kwamba zimepata "taarifa ya huzuni ya kushikiliwa mateka kwa viongozi wa Burkina Faso ikiwa ni pamoja Rais wa nchi hiyo, kitendo ambacho kimefanywa na kikosi cha Usalama wa Rais."

" Taasisi tatu zinalaani ukiukaji wa wazi wa Katiba na Mkataba wa Mpito. Taasisi hizo zinaomba vikosi vya ulinzi na usalama kukabidhi mamlaka ya kisiasa na, katika mazingira ya sasa, kwa viongozi wa mpito ", tangazo hilo limebaini.

Baraza la Usalama pia limelaani kitendo hiki cha kuwateka nyara viongozi kadhaa wa Burkina Faso, akiwemo Rais wa Burkina Faso Michel Kafando na Waziri Mkuu Isaac Zida. baraza hilo linaomba viongozi hao waachiliwe huru mara moja bila masharti.

Kwa sasa, ni vigumu kujua nini kinaendelea ndani majengo hayo. Rais wa mpito, Michel Kafando na Waziri Mkuu Isaac Zida na Mawaziri kadhaa wa serikaliwako mikononi mwa wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa taasisi za uongozi wa nchi. Hakuna madai hadi sasa ambayo yametolewa na kundi hili la wanajeshi.

Mahusiano si mazuri kati ya Waziri Mkuu Isaac Zida, kutoka jeshi, na wanajeshi wa Kikosi cha usalama wa Rais. Migogoro mingi - mwezi Desemba, Februari na Juni - ilitokea kati ya Isaac Zida marafiki zake wa zamani. Na kuingilia kijeshi kwa wanajeshi hao kunakuja wakati ambapo Jumatatu wiki hii, tume ya maridhiano na mageuzi iliyoteuliwa katika kipindi cha mpito ilitoa ripoti yake, ambayo inataka hasa kuvunjwa kwa kikosi cha usalama wa rais (RSP). Je, kuna uhusiano ya moja kwa moja kati ya matukio haya? Kwa sasa, bado ni vigumu kusema kwani madai ya askari wanawashikilia viongozi hao hayajulikani.

Kuingilia huko kwa wanajeshi wa RSP pia kunakuja wiki chache kabla ya uchaguzi wa rais na wabunge, uliyopangwa kufanyika Oktoba 11 kama sehemu ya mchakato wa mpito, ambayo ilianza baada ya kuanguka kwa utawala wa Blaise Compaoré, Oktoba 31 mwaka 2014, baada ya miaka 27 akiwa madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.