Katika makala hii tunazungumzia hatua ya Wabunge nchini Rwanda kupitisha muswada utakaoidhinisha kubadilishwa kwa vipengee vya katiba vitakavyoruhusu rais Paul Kagame kuongoza kwa muhula wa tatu.Katika bunge lililokuwa limejaa wabunge na wananchi waliofurika kushuhudia mjadala huo bungeni, walishangilia na kulitaja jina la rais Kagame baada ya wabunge wote katika baraza la seneti na bunge kupitisha muswada huo kama hatua ya mwanzo kuelekea kufanyika mabadiliko ya katiba.Katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita mamilioni ya raia nchini Rwanda wamekuwa wakitia sahihi pendekezo la kumtaka rais Kagame kuendelea kuongoza taifa hilo hata baada ya kukamilika kwa muhula wake wa pili.