Pata taarifa kuu
Nigeria-Boko haram-Jeshi-Usalama

Nigeria yachukua uongozi wa jeshi dhidi ya Boko Haram

Muhammadu Buhari, rais mpya wa Nigeria, ameonyesha Alhamisi wiki hii nia yake ya kuchukua hatamu ya uongozi wa jeshi dhidi ya wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram. Buhari ameomba marais wenzake wa nchi tano kutoka Ukanda wa Afrika Magharibi kuchukua uongozi wa jeshi la Ukanda huo wakati wote wa “juhudi za vita”.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, katika mkutano wa kilele Abuja kuhusu vita dhidi ya Boko Haram, Abuja Juni 11 mwaka 2015.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, katika mkutano wa kilele Abuja kuhusu vita dhidi ya Boko Haram, Abuja Juni 11 mwaka 2015. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Mbali na nia hii, mkutano wa Abuja, ambao umewaleta pamoja marais wa nchi nyingine za muungano ikiwa ni pamoja na Cameroon, Chad, Niger na Benin, umetoa idadi ya mapendekezo.

Katika mkutano huo kumeanzishwa katika hali ya ufanisi uongozi wa jeshi la pamoja kutoka nchi hizo tano. Yakiwa yalizindiliwa rasmi Mei 25, makao makuu ya kikosi hicho ni ya muda mpaka sasa. Karibu dola milioni 30 zinahitajika ili kikosi hiki kihamiye katika majengo mapya, ambayo yatakua kama makao yake makuu.

Nchi hizi tano pia zimekubaliana kuwatuma wanajeshi wao kabla ya tarehe 30 Julai mwaka 2015. Kikosi hiki, kama ilivyopangwa, kitakua chini ya uongozi wa afisa wa jeshi kutoka Nigeria, meja jenerali Buratai. Naibu mkuu wa kikosi atakua raia wa Cameroon, na kila mwaka uongozi utakua ikibadilishwa. Mkuu wa majeshi atakua afisa wa ngazi ya juu kutoka Chad, na kila mwaka kutakua mabadiliko kwenye nafasi hii.

Inabakia kupata fedha kwa ajili ya kutuma wanajeshi kwa minajili ya operesheni endelevu. Wakuu wa Nchi za Bonde la Ziwa Chad na Benin wametolea wito Umoja wa Afrika kuwapatishia fedha hizo, na pia wameomba msaada wa Umoja wa Ulaya, Ufaransa, Uingereza na Marekani. Marais hao hatimaye wameomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuonyesha, katika tangazo lake, uungwaji wake mkono kwa vita dhidi ya Boko Haram.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.