Pata taarifa kuu
DRC-UNSC-MONUSCO-USALMA

DRC: MONUSCO yaongezewa muda wa mwaka mmoja

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuviongezea muda wa mwaka mmoja wa ziada vikosi vya kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO.

Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiwa pamoja na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, Monusco katika wilaya ya Beni, Desemba 3 mwaka 2014.
Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakiwa pamoja na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, Monusco katika wilaya ya Beni, Desemba 3 mwaka 2014. MONUSCO/Abel Kavanagh
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo idadi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itapunguzwa kwa kiwango cha asilimia 10 sawa na wanajeshi 2000.

Serikali ya Kinshasa ilikua ikiomba Umoja wa Mataifa kupunguza idadi ya wanajeshi wake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Umoja wa Mataifa una zaidi ya wanajeshi 19 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, idadi ambayo ni kubwa ikilinganishwa na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani katika mataifa yanayokumbwa na machafuko duniani.

Hata hivyo serikali ya Kinshasa imekua ikiomba kupunguzwa kwa wanajeshi 6000 wa Umoja wa Mataifa nchini katika nchi yake tangu mwaka 2015, lakini Umoja wa Mataifa umekua ukisema kwamba bado ni mapema mno kupunguza idadi ya wanajeshi wake. Mdororo wa kiusalama bado unaripotiwa katika baadhi ya maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hivi karibuni zaidi ya watu 40 waliuawa katika mji wa Kinshasa katika maandamano ya kupinga Bunge na Baraza la Seneti kufanya marekebisho ya baadhi ya Ibara ili kumpa nafasi rais Joseph Kabila kugombea muhula mwengine.
Zaidi ya makundi thelathi ya watu wenye silaha bado yanaendelea kuhatarisha usalama wa raia hususan mashariki mwa nchi hio pamoja na hali ya sintofahamu ambayo imekua ikiripotowa mara kwa mara katika mkoa wa Katanga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.