Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mshukiwa wa shambulio la Bamako auawa na polisi

Vikosi vya usalama vya Mali vimesema kwamba vimemuua mmoja kati ya washukiwa wa shambulio lililotekelezwa Ijumaa wiki iliyopita dhidi ya ya mgahawa La terasse katika mji mkuu wa Mali, Bamako.

Polisi imefunga mta wa Princess ambako kunapatikana mgahawa La Terrasse (jengo lenye mapazia ya bluu), eneo kulikotokea shambulio la risasi lililosababisha maafa,  usiku wa tarehe 6 Mach kuamkia Machi 7 mwaka 2015.
Polisi imefunga mta wa Princess ambako kunapatikana mgahawa La Terrasse (jengo lenye mapazia ya bluu), eneo kulikotokea shambulio la risasi lililosababisha maafa, usiku wa tarehe 6 Mach kuamkia Machi 7 mwaka 2015. AFP PHOTO / SEBASTIEN RIEUSSEC
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo liligharimu maisha ya watu watano ikiwa ni pamoja na raia watatu wa Mali, mmjo kutoka Ubelgiji na raia mmoja wa Ufaransa. Shambulio lilidaiwa kuendeshwa na kundi la Al mourabitoune linaloongozwa na raia wa Algeria Mokhtar Belmokhtar.

Kwa mujibu wa waziri wa wa mambo ya ndani wa Mali, vikosi maalumu vya Idara ya Ujasusi vya Mali vimemuua mmoja wa washukiwa hao leo Ijumaa asubuhi, katika operesheni iliyoendeshwa na vikosi hivyo. Vikosi vya usalama viliwasili eneo la tukio Alhamisi jioni kabla ya saa sita usiku.

Afisa mwandamizi wa vikosi maalumu vya Idara ya Ujasusi vya Mali amebaini kwamba walikua na taarifa za uhakika.

“ Tulipata taarifa za uhakika, na tuliweza kumdhibiti mtu huyo ambaye alirusha gruneti katika mtaa kunakopatikana mgahawa La Terasse katika mji wa Bamako Jumamosi iliyopita”, amesema afisa huyo, akibaini kwamba mtu huyo alikua alijificha katika jengo moja mjini Bamako.

“ Tulimtaka kufungua mlango kwa sababu alikuwa akifuatiliwa tangu siku kadhaa. Mtu huyo baadae alirusha gruneti mbele ya mlango, bahati mbaya ameuawa na wanajeshi wetu watatu wamejeruhiwa katika operesheni hiyo”, ameongeza afisa huyo.

Kwa mujibu wa mashahidi waliohojiwa na RFI eneo la tukio, milio mingi ya risasi ilisikika.

Maasfisa wa usalama wamebaini kwamba wamemkuta mshukiwa huyo na kadi ya uraia ambayo ni bandia. Kwenye kadi hiyo inaonesha kuwa mshukiwa huyo anaitwa Mohamed Tamirou Cissé. Na inaonesha pia kuwa alizaliwa mwaka 1993 katika kijiji cha Moudakam, katika mji wa Bourem, kaskazini mwa Mali. Watuhumiwa wenza bado wanatafutwa na polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.