Pata taarifa kuu
NIGER-BOKO HARAM-MAUAJI-USALAMA

Niger yapoteza wanajeshi 7 katika mapigano dhidi ya Boko Haram

Wanajeshi saba wameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa katika mapigano yaliyotokea katika kijiji kiliyo karibu na Ziwa Chad, baada ya kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram.

wanajeshi wa Nigeria wakikabiliana na wapiganaji wa Boko Haram. Mbali kidogo na wanajeshi hao, kunaonekana bendera ya kundi la Boko Haram.
wanajeshi wa Nigeria wakikabiliana na wapiganaji wa Boko Haram. Mbali kidogo na wanajeshi hao, kunaonekana bendera ya kundi la Boko Haram. RFI/ Nicolas Champeaux
Matangazo ya kibiashara

Kijiji hicho kilishambuliwa Ijumaa jioni Februari 20 na wanamgambo wa kundi hilo la Boko Haram, jeshi la Niger limethibitisha katika tangazo lililotoa Jumamosi wiki hii. Hata hivyo wanamgambo 14 wa Boko Haram waliuawa katika mapigano hayo, limeongeza jeshi la Niger.

Kundi la Boko Haram limeendelea kukabiliana na majeshi kutoka Niger, Cameroon, Nigeria na Chad, huku kundi hili likiendelea kuhujumu raia katika maeneo mbalimbali ya nchi hizi ziliyoanzisha vita dhidi ya Boko Haram.

Miezi ya hivi karibuni Chad ilituma wanajeshi wake nchini Cameroon ili kukabiliana na Boko Haram, ambayo ilikua ikiendesha mashambulizi ya mara kwa mara katika vijiji vinavyopakana katika nchi hizi nne.

Hivi karibuni watu 36 waliuawa katika mji mdogo wa Niger wa Abadam, unaopakana na Nigeria, kwenye umbali wa kilomita zaidi ya kumi na mbili, na wengine zaidi ya ishirini walijeruhiwa katika shambulio la bomu lilioendeshwa na ndege isiyojulikana.

Watu hao walikua katika sherehe za mazishi katika Msikiti mmoja wa mji huo wa Abadam.

Abadam ni kijiji kinachopatikana kwenye mpaka na Nigeria. Sehemu mmoja ya Abadam upande wa Nigeria ilikua ikikaliwa na wanamgambo wa Boko Haram, miezi kadhaa iliyopita. Hata hivyo wakazi wa sehemu hiyo wamekua wakitiwa hofu na hali hio inapofika usiku, wengi wamekua wakilala msituni, na wanarejea inapofika asubuhi.

Ndege isiyojulikana ilishambulia Msikiti mmoja wa kijiji hicho Jumanne wiki hii, wakati walikua katika sherehe za mazishi, upande wa Niger. Zaidi ya watu 30 walikua katika Msikiti wakitoa hashimu za mwisho kwa mzee mmoja aliyefariki siku tatu zilizopita.

Nigeria iliendesha shambulio dhidi ya wapiganaji wa Boko Haram waliokua eneo hilo tangu miezi minne iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.