Pata taarifa kuu
KENYA-ODINGA-USALAMA

Kifo cha Fidel Odinga chasikitisha Wakenya

Mtoto wa kwanza wa Waziri mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga, alifariki usiku wa Jumamosi Januari 3 kuamkia Jumapili Januari 4 katika mazingira ambayo hayajawekwa bayana.

Nairobi, mji mkuu wa Kenya, ambako Fidel Odinga, alikutwa amekufa.
Nairobi, mji mkuu wa Kenya, ambako Fidel Odinga, alikutwa amekufa. AFP PHOTO / SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Fidel Odinga, alikuwa akirudi nyumbani usiku katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Raia wa Kenya wametoa hisia tofauti kufuatia kifo cha Fidel Odinga ambaye amekua akionekana kama mrithi wa baba yake katika siasa.

Fidel Odinga alikutwa amekufa nyumbani kwake katika kata ya Karen, ambako alikua akiishi na mke wake wa pili mwenye asili ya Eritrea na mtoto wao mdogo.

Fidel Odinga alikua akirudi nyumbani usiku wa manane akitokea katrika burudani na marafiki zake katika hoteli Sankara katika eneo la Westlands.

Baada ya taarifa ya kifo chake, hisia mbalimbali zimetolewa na wanasiasa kutoka makundi mbalimbali. Rais Uhuru Kenyatta, kama watangulizi wake Mwai Kibaki na Daniel Arap Moi, walisikitikia kifo cha kijana huyo , ambaye alikua akipewa nafasi kubwa ya kumrithi baba yake katika siasa nchini Kenya.

Kalonzo Musyoka, aliyekuwa mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi mkuu wa mwezi Machi mwaka 2013, ametolea wito polisi kuharakia kufanya uchunguzi ili kujua haraka iwezekanavyo sababu za kifo chake.

Jumapili Januari 4 mwaka 2015 mchana, mamia ya wakazi wa kitongozi cha Kibera wameonyesha hasira zao na kubaini kutoelewa kuhusu kutokea kwa kifo cha Fidel Odinga. Fidel Odinga alikua na nia ya kugombea katika uchaguzi wa mwaka 2017.

Mtoto huyo wa kwanza wa Raila Odinga, alizaliwa mwaka 1973, na aliitwa jina la Fidel kwa heshima ya Fidel Castro, rais wa zamani wa Cuba, wakati baba yake na babu yake walikuwa wote walidhamiria katika itikadi za kikomunisti.

Fidel Odinga ambaye ni miongoni mwa watoto wanne wa Raila Odinga, alikua akipewa nafasi kubwa ya kumrithi kisiasa baba yake.

Hayo yakijiri, mtu mmoja amefariki na wengine kujeruhiwa baada ya jumba la makazi la ghorofa saba kuporomoka katika mtaa wa Huruma jijini Nairobi nchini Kenya.

Maafisa wa uokoaji wa jiji la Naiorobi wanasema, watu zaidi ya 20 wameokolewa lakini haijafahamika ni watu wa ngapi waliokuwa katika jengo hilo.

Ripoti zinasema kuwa, ghorofa sita zilikuwa makazi ya watu na ghorifa ya saba ilikuwa inaendelea kujengwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.