Pata taarifa kuu
MALI-UN-USALAMA

Mkuu wa kikosi cha UN Mali amaliza muda wake

Jenerali Jean-Bosco Kazura, ambaye kwa kipindi cha miezi 18 alikua akihudumu kwenye kikosi cha Umoja wa mataifa nchini Mali (Munusma) kama mkuu wa kikosi hicho, amemaliza muda wake, na kuamua kuachia ngazi.

Jenerali Jean-Bosco Kazura, mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali, ambaye ameamua kuachia ngazi.
Jenerali Jean-Bosco Kazura, mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali, ambaye ameamua kuachia ngazi. David Baché / RFI
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hii imeshangaza wengi, wakati ambapo jina la atakaye mrudilia halijafahamika rasmi.

Jenerali Jean Bosco Kazura ni afisa wa ngazi ya juu katika jeshi la Rwanda. Amesema ameamua kuachia ngazi kwa sababu zake binafsi.

Jenerali Jean-Bosco Kazura aliteuliwa kwenye nafasi hiyo mwezi Juni mwaka 2013.

Jenerali Jean Bosco Kazura anajulikana kutokana na ujasiri wake. Amekamilisha kazi yake mjini Bamako baada ya miezi 18 akiwa mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali, kikosi ambacho kina jumla ya askari wa kulinda amani 8,000.

Rekodi yake ina dosari, lakini si kosa lake. Jukumu la askari wa Umoja wa Mataifa haliko imara. Kwa hiyo, kwenye uwanja wa vita, kikosi hicho hakina uwezo wa kukabiliana na mbinu za wanamgambo wa kiislam.

Kikosi cha Umoja wa mataifa nchini Mali kilipotza askari wengi, baada ya kushambuliwa na wapiganaji wa kiislam katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Katika kipindi cha miezi 16, zaidi ya askari thelathini wa kikosi cha Umoja wa Mataifa kutoka Chad, Burkina Faso na Niger waliuawa.

Hata hivyo Chad imekua ikitishia kuwaondoa wanajeshi wake nchini Mali kufuatia mashambulizi dhidi yao. Marais wa Niger na Mali kwa upande wao, waliomba kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali kuonesha uwezo wao kwenye uwanja wa mapambano.

Jenerali Jean-Bosco Kazura, anatazamiwa kujielekeza Jumanne Desemba 9 mjini New York kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ili kufikisha ripoti ya kazi aliyoifanya nchini Mali kwa kipindi cha miezi 18 kama mkuu wa kikosi cha Umoja wa mataifa (Minusma).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.