Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAREKANI-BOKO HARAM-Diplomasia-Usalama

Mvutano wa kidiplomasia kati ya Nigeria na Marekani

Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Nigeria na Marekani yameingia kasoro. Sehemu ya mwisho ya kuongezeka mvutano katika mahusiano kati ya nchi hizo mbili: Nigeria kusitisha mafunzo yaliyokua yakitolewa na Marekani kwa kikosi cha jeshi la Nigeria ili kupambana dhidi ya kundi la Boko Haram.

Zoezi la pamoja kati ya majeshi ya Nigeria na Marekani katika mji wa Lagos Oktoba 18 mwaka 2013.
Zoezi la pamoja kati ya majeshi ya Nigeria na Marekani katika mji wa Lagos Oktoba 18 mwaka 2013. AFP PHOTO/ PIUS UTOMI EKPEI
Matangazo ya kibiashara

Ushirikiano huu ulianzishwa kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi ya kundi hilo la Boko Haram pamoja na kitendo cha kuwateka nyara wasichana zaidi ya 200 katika mji wa Chibok mwezi Aprili mwaka 2014.

Kwa ombi la Abuja, Marekani imesitisha mafunzo hayo kwa kikosi cha jeshi la Nigeria. Uamzi huo umetangza kupitia tangazo lililotolewa Jumatatu Desemba 1 jioni na ubalozi wa Marekani, ambapo Marekani ilichukua uamzi wa kusitisha ushirikiano wa kijeshi na Nigeria kwa muda wa miezi.
Awamu mbili za kwanza za mafunzo zilikamilika kati ya mwezi Aprili na Agosti. Awamu ya tatu ingeliwezesha jeshi la Nigeria kupata uwezo wa kupambana na Boko Haram.

Ila kwa kuwa mvutano umekuwa ukikua kwa pande zote mbili, mafunzo hayo yamesitishwa. Mwezi uliopita, balozi wa Nigeria mjini Washington alisema serikali yake inaona kuwa msaada wa Marekani kwa nchi yake hautoshi.

Balozi huyo aliikosoa Marekani kukataa kuiuzia Nigeria silaha na vifaa mbalimbali vya kijeshi. wizara ya ulinzi ya Marekani ilikua imeshaonyesha wasiwasi juu ya ukiukwaji wa mara kwa mara unaotekelezwa na askari wa Nigeria pamoja na uwezo wa kijeshi kwa kulinda raia.

Kwa kweli, Marekani imekua ikinyooshea kidole kashfa ya rushwa ambayo imekithiri katika jeshi la Nigeria. Licha ya Euro bilioni 4.9 zilizotengwa kwa ajili ya ulinzi, sawa na asilimia 20 ya bajeti ya serikali, vikosi vya usalama vimekua vikijihusisha na rushwa na kupaka matope serikali ya Nigeria.

Jeshi la Nigeria linakabiliwa na ukosefu wa vifaa, mshahara hafifu, na hizo ni baadhi ya sababu zinazopelekea jeshi la Nigeria kushindwa kupambana na kundi la Boko Haram. Hata hivyo hazina za jeshi haziwezi kaguliwa, kwa sababu itakua ni kuingilia undani wa siri za jeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.