Pata taarifa kuu
FDLR-RWANDA-DRC

FDLR yarejesha silaha kwa mwendo wa kinyonga

Silaha 600 ziliyorejeshwa na makundi mbalimbali yenye silaha kutoka nchini Congo na yale kutoka nchi za kigeni na kuzikabidhi tume ya Umoja wa Mataifa Monusco, zimechomwa moto Ijumaa Novemba 28 kwenye makao makuu ya Monusco mjini Goma.

Wanamgambo wa FDLR wajisalimisha katika kijiji cha Kateku mashariki mwa DRC, Mei 30 mwaka 2014.
Wanamgambo wa FDLR wajisalimisha katika kijiji cha Kateku mashariki mwa DRC, Mei 30 mwaka 2014. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Viongozi mbalimbali katika jeshi na utawala wa mkoa wa Kivu Kaskazini pamoja na naibu katibu wa Umoja wa mataifa anayehusika na masuala katiba za usalama walikuepo. Silaha nyingi zilitoka mukononi mwa waasi wa kihutu wa Rwanda wa FDLR.

Zoezi la kupokonya silaha kwa nguvu linatazamiwa kuanza ndani ya mwezi mmoja. Waasi wa kihutu wa Rwanda walikua walipinga kuresha silaha. Hatimaye baadhi yao wamekubali kuondoka katika mkoa wa Kivu Kaskazini, na wamewasili katika mji wa Kisangani ili waweze kupokonywa silaha na warejeshwe katika maisha ya kiraia.

Awali waasi hao walikua walikataa kurejesha silaha na kupelekwa Kisangani, wakihofia usalama wao. Hata hivyo, si waasi wote wa kihutu wa Rwanda wanaoendesha harakati zao mashariki mwa Congo ambao wako tayari kuondoka katika mkoa wa Kivu Kaskazini, kama unavyoeleza mpango waliyokubaliana na jumuiya ya kimataifa

Hayo yakiri, waasi wengine wa kihutu wa Rwanda wamekua wakiiomba serikali ya Kigali kuanzisha mazungumzo yatakayowashirikisha raia wote wa rwanda wakiwemo waasi hao, ombi ambalo serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilisema haikubaliani nalo, ikibaini kwamba kwa sawa ni vigumu kuishawishi serikali ya Kigali kuanzisha mazungumzo na FDLR. Kinshasa ilibaini kwamba usalama wa raia wa Congo ndio unapaswa kupewa kipaombele, kwani wao ndio walengwa wa kwanza na waasi hao wa kihutu wa Rwanda.

Mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka 2015, jeshi la Congo (FARDC) likisaidiwa na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Mataifa (monusco) wanatazamia kuanza operesheni ya kuwapokonya silaha kwa nguvu waasi hao wakihutu wa Rwanda. Uamzi huo ulithibitishwa na katika mkutano wa Jumuiya ya nchi za ukanda wa maziwa makuu uliyofanyika hivi karibuni mjini Luanda, nchini Agola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.