Pata taarifa kuu
BURUNDI-RWANDA-MAREKANI-FBI-Haki za binadamu

Burundi: Maiti ziliyogunduliwa katika ziwa Rweru zilitokea Rwanda

Kwa muda wa miezi mitatu, utata umekua ukijitokeza kati ya serikali ya Burundi na Kigali kuhusu maiti ziliyogunduliwa katika ziwa Rweru liliyo kati ya Burundi na Rwanda.

Bandari ndogo ya wavuvi wa Burundi kwenye ziwa Rweru, ambapo kulizikwa maiti ziliyogunduliwa katika ziwa hilo.
Bandari ndogo ya wavuvi wa Burundi kwenye ziwa Rweru, ambapo kulizikwa maiti ziliyogunduliwa katika ziwa hilo. RFI / Esdras Ndikumana
Matangazo ya kibiashara

Mwendesha mashtaka mkuu wa taifa nchini Burundi, ametangaza jana Jumanne mbele ya vyombo vya habari matokeo ya mwanzo ya uchunguzi uliyoendeshwa na idara yake na kubaini kwamba maiti hizo zilitokea nchini jirani ya Rwanda.

Awali viongozi wa Burundi walitangaza kwamba waliunda tume ya mseto inayoundwa na wajumbe kutoka Burundi na Rwanda ili waweze kuanzisha uchunguzi kuhusu miili hiyo ya watu iliyogunduliwa katika ziwa Rweru.

Ukweli umeanza kudhihirika baada ya Mewendesha mashtaka muu wa taifa nchini Burundi, Valentin Bagorikunda, kuweka wazi baadhi ya mambo kuhusu miili hiyo.

Bagorikunda amesema miili minne ya watu iliyogunduliwa hivi karibuni katika ziwa Rweru ilitokea Rwanda . Hata hivyo yombo vya habari vilikua vikibaini kuwa hakuna uchunguzi unaoendeshwa tangu ilipodundulika miili hiyo ya watu, miezi miwili iliyopita. Lakini Mwendesha mashataka huyo wa taifa nchini Burundi, amethibitisha kuwa uchunguzi uliendeshwa na matokeo yake yametokana na uchunguzi huo.

Kiongozi huyo mkuu wa ofisi ya mashtaka nchini Burundi amesema matokeo hayo yametokana na uchunguzi uliyoendeshwa katika eneo kulikogunduliwa miili hiy, ripoti za vyombo mbalimbali vya usalama, ripoti za viogozi tawala kwenye ngazi ya mkoa na wilaya nchini Burundi, pamoja na ushahidi uliyotolewa na wakulima na wavuvi kutoka Burundi na Rwanda ambao wanaendesha shughuli zao katika ziwa Rweru na mto Akagera uliyo karibu na ziwa hilo.

Valentin Bagorikunda amebaini kwamba wanachohitaji kwa sasa ni kuwatambuwa raia hao waliouawa, akisema kwamba polis ya Burundi haina uwezo. Hata hivo serikali ya Burundi ilifahamaisha hivi karibuni kwamba kuna uwezekano Kikosi cha Marekani cha FBI kitowe ushiriki wake katika uchunguzi huo. Lakini kauli hii imebadilishwa: “ Kwa sasa uchunguzi umekamilika, tunacho hitaji ni kutambua watu hao waliyouawa", amesema Bagorikunda .

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeielezea RFI kwamba imeanza mazungumzo na serikali za nchini hizo mbili husika “ kuhusu utaratibu unaohitajika kwa kuendesha uchunguzi wa kimataifa. Wizara hiyo ya Marekani imebaini kwamba haijaombwa na taifa lolote ili itowe ushiriki wake katika uchunguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.