Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-SADC-Siasa

Madagascar: Ravalomanana akamatwa baada ya kuwasili Antananarivo

Rais wa zamani wa Madagascar, Marc Ravalomanana amekamatwa baada ya kuwasili mjini Antananarivo akitokea uhamishoni Afrika kusini.  

Rais wa zamani wa Madagascar, Marc Ravalomanana, Februari 17 mwaka 2011.
Rais wa zamani wa Madagascar, Marc Ravalomanana, Februari 17 mwaka 2011. Reuters / Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Haijabainika ni sababu gani ziliyopelekea rais huyo wa zamani wa Madagascar anakamatwa. Marc Ravalomana amekamatwa akiwa nyumbani kwake. Kabla ya kukamatwa, Marc Ravalomanana amewambiwa Jumatatu asubuhi wiki hii kwamba kwamba bado ana mamlaka kwani amerejea nchini wakati alikua hana pasipoti ya usafiri.

Polisi imewatawanya wafuasi wa rais huyo wa zamani kabla ya kukamata. Lakini ikulu ya Antananarivo imebaini kwamba haikua na taarifa yoyote kuhusu kurejea kwa Marc Ravalomanana jumatatu wiki hii..

Afisaa mmoja kwenye Ikulu ya Antananarivo amesema kuwa Marc Ravalomanana amerejea bila hata hivo serikali kuwa na taarifa yoyote, akibaini kwamba huenda amepenya na kuingia nchini kinyume cha sheria.

Marc Ravalomanana alitimuliwa madarakani kufauatia jaribio la mapinduzi ya kijeshi mwaka 2009 kwa niaba ya Andry Rajoelina, meya wa zamani wa mji wa Antananarivo, na baadaye alichukua madaraka baada ya mapinduzi hayo.

Marc Ravalomanana amewasili Jumatatu asubuhi wiki hii mjini Antananarivo akiwa katika ndege ya kibinafsi iliyokodiwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC.

Muda mfupi tu baada ya kuwasili jijini Antananrivo, kiongozi huyo wa zamani amejikuta pabaya baada ya kutakiwa kuripoti mahakamani na kuwekwa kuzuizini muda tu baada ya kuwasili nchini humo.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na ndugu zake, na baadaye kuthibitishwa na kiongozi wa ujumbe aliyokuja nao, Marc Ravalomanana aliondoka Afrika Kusini usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu.

Marc Ravalomanana amezunguza kwa mara ya kwanza na wafuasi wake, baada tu ya kuwasili katiuka mji mkuu wa Madagascar, Antananarivo.

Rais huyo wa zamani wa Madagascar alijaribu kurejea nchini mara kadhaa bila mafanikio.

Jumamosi iliyopita, Marc Ravalomanana aliwaonya wafuasi wake kutokusanyika katika uwanja atakaporudi, moja ya masharti aliyopewa na utawala uliko sasa madarakani nchini Madagascar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.