Pata taarifa kuu
TANZANIA-POLISI-WAANDISAHI-Haki za binadamu

Tanzania: wanahabari wazuiliwa kuendesha kazi yao

Waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, nchini Tanzania wamekabiliwa alhamisi wiki hii na kibarua kigumu baada ya kujikuta wakizuiliwa na polisi wakiwa katika kazi yao ya kuripoti habari.

Mji wa Dar es Salaam, nchini Tanzania.
Mji wa Dar es Salaam, nchini Tanzania. Wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limetokea wakati waandishi wa habari walipokuwa katika shughuli zao za kutafuta habari wakati mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini humo cha Chadema Freeman Mbowe alipowasili katika ofisi za makao makuu ya polisi kutokana na tuhuma zinazo mkabili za uchochezi kuhusu kauli yake ya kuitisha maandamano nchi nzima.

Polisi nchini Tanzania ililazimika kufunga barabara inayoelekea kwenye ofisi za makao makuu ya polisi kutokana na wafuasi wa Chadema waliokuwa wamefurika kwa wingi katika eneo hilo, jambo ambalo linadaiwa kuwa kinyume cha sheria.

Hata hivyo waandishi wa habari ambao walikuwa wamejielekeza katika eneo hilo kwa ajili ya kuripoti habari hawakurahisishiwa na polisi na kujikuta polisi ikikabiliana nao kuwafurusha katika eneo hilo, huku wengine wakidai kunyanyaswa na Polisi.

Baraza la wahariri nchini Tanzania limsema tukio hili linaskitisha kutokea siku chache baada ya mkutano wa vyombo vya dola na waandishi wa habari.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.