Pata taarifa kuu
UGANDA-Ushoga-Sheria

Uganda: Sheria ya ushoga yafutwa

Korti ya kikatiba nchini Uganda imefuta sheria dhidi ya mashoga iliyotiliwa saini na rais Yoweri Kaguta Museveni Februari mwaka 2014, ikibaini kwamba wabunge waliyoidhinisha sheria hiyo hawakutimiza idadi iliyokua inahitajika.

Wanaharakati wa haki za mashoga wapongeza kufutwa kwa sheria dhidi ya ushoga Uganda.
Wanaharakati wa haki za mashoga wapongeza kufutwa kwa sheria dhidi ya ushoga Uganda. REUTERS/Edward Echwalu
Matangazo ya kibiashara

“ Sheria dhidi ya ushoga imefutwa na haina nguvu tena kwa kuwaadhibu mashoga”, amesema mkuu wa korti ya kikatiba.

Sheria hiyo imekua imepiga marufuku mapenzi ya watu wa jinsia moja na kuwataka raia kuwafichua watu wote wanaojihusisha na kitendo hicho cha ushoga. Adhabu ya kifungo cha maisha jela ilikua inamkabili mtu anaye jihusisha na ushoga, adhabu ambayo ililalamikiwa na jumuiya ya kimataifa. Wafadhili wengi wa Uganda walifuta baadhi ya misaada waliyokua wakiitolea serikali ya nchi hiyo.

Kufutwa kwa sheria hiyo kumepongezwa na wanaharakati wa haki za mashoga.

“ Sheria dhidi ya ushoga kwa sasa haina kazi tena”, amesema akipongeza Andrew Mwenda, ambaye ni mwanahabari akiwa pia mwanaharakati

Kassisi Martin Ssempa, anaepinga ushoga, amesema Marekani itasababisha Uganda inakumbwa na lana kama ile ya Sodoma na Gomora, akilani vikwazo viliyochukuliwa na Marekani dhidi ya Uganda kufuatia kupitisha sheria dhidi ya ushoga.

Kasisi huyo, akivalia joho amefanya ibada ya dakika chache ndani ya korti kulikokua kumejaa watu wakisubiri uamzi wa majaji, ili kutaka majaji wasifute sheria hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.