Pata taarifa kuu
MALI

Makundi yenye silaha nchini Mali yakiri kuwa tayari kwa mazungumzo ya amani na Serikali

Makundi yenye silaha kaskazini mwa Mali yameelezwa kuwa tayari kwa mazungumzo ya amani na Serikali ili kumaliza machafuko yanayoshuhudiwa kaskazini mwa nchi hiyo, waziri wa mambo ya kigeni wa Algeria amethibitisha.Hayo yanajiri wakati wanadiplomasia wa kimataifa wamesema kuwa waasi wa kundi la Tuareg wanaotaka kujitenga walikubali kusitisha vita mwishoni mwa mwezi uliopita,  baada ya kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa umoja wa afrika Mohammed Abdel Azizi mjini Kidal.

Kamanda mkuu wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu Aliou Mohamed, na mkuu wa Mji wa Gao, akiinua silaha mtindo wa PM AK 47.
Kamanda mkuu wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu Aliou Mohamed, na mkuu wa Mji wa Gao, akiinua silaha mtindo wa PM AK 47. RFI
Matangazo ya kibiashara

Waziri Ramtane Lamamra amethibitisha kupokea maombi ya barua toka kwa makundi matatu ya kaskazini mwa nchi ya Mali ambayo yameonesha nia ya kutaka kuwa na suluhu na Serikali kuhusu maeneo ya kaskazini.

Waziri Lamamra ametoa kauli hii wakati wa mkutano uliowakutanisha mawaziri toka mataifa sita ya ukanda wa Sahel, ikiwemo Niger, Mali, Burkinafaso, Mauritania na Chad pamoja na mwakilishi wa Umoja wa Afrika na rais wa zamani wa Burundi, Pierre Buyoya, ambapo viongozi hawa wamekubaliana kuandaa mpango utakaoshuhudia mazungumzo hayo yakianza.

Kauli ya waasi hao inakuja baada ya ripoti za mashirka ya kimisaada yaliyoko nchini Mali kuripoti kuwa takriban wanajeshi 20 wa Mali walipoteza maisha baada ya jaribio la kutaka kuuteka mji wa kaskazini mwa Mali wa Kidal kutoka kwa waasi hao kufeli,
Waasi hao wanadhibiti eneo lote la kazkazini mashariki mwa Mali na sasa wanaelekea katika mji wa Gao.

Serikali imewashtumu waasi hao kwa kuungwa mkono na wapiganaji wa kundi la Al Qaeda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.