Pata taarifa kuu
MALAWI-Siasa-Uchaguzi

Peter Mutharika atangazwa mshindi wa kiti cha Uraisi

Peter Mutharika ndugu wa raisi wa zamani Bingu wa Mutharika ametangazwa mshindi wa kiti cha uraisi nchini Malawi baada ya kushuhudia uchaguzi ulifanyika hivi karibuni.Kiongozi huyo wa chama cha DPP amepata asilimia 36.4 ya kura zote Tume ya uchaguzi Malawi imetangaza.

Peter Mutharika,ndugu wa raisi Bingu wa Mutharika aibuka mshindi wa kiti cha uraisi Malawi
Peter Mutharika,ndugu wa raisi Bingu wa Mutharika aibuka mshindi wa kiti cha uraisi Malawi AFP PHOTO / AMOS GUMULIRA
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la polisi nchini Malawi limetumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya raia kadhaa wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa chama cha raisi Joyce Banda waliojitokeza katika jiji la kusini mashariki Mangochi hii leo wakati huu homa ya matokeo ya uchaguzi ikipanda baada ya zoezi la kupiga kura kutamatika juma lililopita.

Zaidi ya mamia ya raia wamechoma magurudumu barabarani katika maeneo ya Mangochi,msemaji wa jeshi la polisi Rodrick Maida ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP.

Polisi imesema inatumia mabomu ya machozi kuwatawanya Watu hao wanaofanya ghasia huku wanasema uchaguzi umegubikwa na wizi.

Kwa mujibu wa polisi waandamanaji mjini Mangochi ni wafuasi wa chama cha raisi Joyce Banda People's Party nafasi ya tatu kwa idadi ya kura za awali.

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Malawi ilisema kuwa zoezi la uchaguzi lililofanyika nchini humo juma moja lililopita lilikuwa huru na haki na amani licha ya kasoro zilizojitokeza, kauli inayotolewa wakati huu tume ya uchaguzi ikijiandaa kutangaza matokeo rasmi hii leo.

Mwenyekiti wa tume hiyo, Maxon Mbendera aliwaambia waandishi wa habari mjini Lilongwe kuwa hana shaka na matamshi yake kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki licha ya malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wagombea kuhusu uchaguzi huo.

Kauli ya tume inakuja wakati ambapo hapo jana mahakama kuu ilishindwa kutoa uamuzi iwapo tume hiyo itangaze matoke leo au la baada ya jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo awali kutangaza kujitoa.

Tayari mahakama hiyo imemteua jaji Healy Potani kusikiliza kesi hiyo na kuitolea uamuzi leo Ijumaa ambapo itafahamika iwapo tume hiyo iatatngaza matokeo au itapewa siku 30 zaidi kuhesabu upya kura nchi nzima.

Hata hivyo kiongozi wa chama cha Democratic Progressive Peter Mutharika, ambaye alionekana kuongoza katika kura za awali alitaka mahakama kuzuia nyongeza ya siku 30.

Kwa upande wake raisi Joyce Banda,ambaye alionekana kushika nambari ya tatu kwa idadi ya kura juma lililopita alisema kuwa uchaguzi huo ni batili kwa kugubikwa na ukiukwaji wa taratibu na kuitisha uchaguzi mpya ndani ya siku tisini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.