Pata taarifa kuu
MALAWI-Siasa-Uchaguzi

Tume ya uchaguzi Malawi yasema uchaguzi ulikuwa huru na haki

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Malawi imesema kuwa zoezi la uchaguzi lililofanyika nchini humo juma moja lililopita lilikuwa huru na haki na amani licha ya kasoro zilizojitokeza, kauli inayotolewa wakati huu tume hiyo ikijiandaa kutangaza matokeo rasmi hii leo.

Raisi Joyce Banda akipiga kura yake 20 May 2014.
Raisi Joyce Banda akipiga kura yake 20 May 2014. REUTERS/Eldson Chagara
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa tume hiyo, Maxon Mbendera amewaambia waandishi wa habari mjini Lilongwe kuwa hana shaka na matamshi yake kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki licha ya malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya wagombea kuhusu uchaguzi huo.

Kauli ya tume inakuja wakati ambapo hapo jana mahakama kuu ilishindwa kutoa uamuzi iwapo tume hiyo itangaze matoke leo au la baada ya jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo awali kutangaza kujitoa.

Tayari mahakama hiyo imemteua jaji Healy Potani kusikiliza kesi hiyo na kuitolea uamuzi leo Ijumaa ambapo itafahamika iwapo tume hiyo iatatngaza matokeo au itapewa siku 30 zaidi kuhesabu upya kura nchi nzima.

Hata hivyo kiongozi wa chama cha Democratic Progressive Peter Mutharika, ambaye alionekana kuongoza katika kura za awali alitaka mahakama kuzuia nyongeza ya siku 30.

Kwa upande wake raisi Joyce Banda,ambaye alionekana kushika nambari ya tatu kwa idadi ya kura juma lililopita alisema kuwa uchaguzi huo ni batili kwa kugubikwa na ukiukwaji wa taratibu na kuitisha uchaguzi mpya ndani ya siku tisini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.