Pata taarifa kuu
Angola-icglr

Viongozi wa Jumuiya ya ukanda wa maziwa makuu wayatuhumu makundi ya uasi mashariki mwa DRCongo

Viongozi wa Jumuiya ya ukanda wa Afrika mashariki na kati wameyatuhumu makundi ya uasi mashariki mwa Jamahuri ya Kidemokrasia ya Congo yanayoendelea kuyumbisha Usalama katika eneo hilo.Hayo ni katika mkutano wa siku mbili uliofanyika jijini Luanda nchini Angola chini ya mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye pia ni rais wa Angola Jose Eduardo Dos Santos

Viongozi wa mkutano wa ICGLR
Viongozi wa mkutano wa ICGLR
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Angola Jose Eduardo Dos Santos ambaye ameongoza kikao kilicho wakutanisha viongozi wa mataifa ya DRCongo, Congo Brazaville, Afrika Kusini, Rwanda, Tanzania na Uganda amesema viongozi wa kijeshi katika eneo hilo wanatakiwa kuhakikisha makundi hayo sio kitisho kwa nchi za ukanda huu.

Rais Santos ametowa wito wa kuyatokomoeza makundi ya ADF Nalu, la waasi wa Uganda waliopiga kambi nchini DRC pamoja na kundi la FDLR la waasi wa kihutu wa Rwanda waliokita mizizi mashariki mwa DRCongo tangu kupinduliwa kwa rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana.

Katika hatuwa hiyo, serikali ya Afrika Kusini imetangaza kuongeza muda wa uwepo wa vikosi vyake vilivyopo chini ya Umoja wa Mataifa nchini DRCongo hadi March 31, mwaka 2015.

Katibu mtendaji wa kikao cha marais wa Jumuiya hiyo ya ICGLR Alphonse Ntumba Lwaba amesema kuna hatuwa za kupongezwa katika kupiga vita makundi hayo kutoka upande wa DRCongo lakini pia na upande wa Rwanda.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.