Pata taarifa kuu
Centrafrica

Samba Panza awakumbusha wanawake jukumu lao la kufanikisha amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Catherine Samba Panza ameshutumu mauaji yanayofanywa dhidi ya wanawake waislamu nchi nzima kutokana na vita ya kidini, 

Rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba Panza
Rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba Panza AFP
Matangazo ya kibiashara

Akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani jana Jumamosi,rais huyo amesema kuwa inatia uchungu mkubwa kuona kuwa baadhi ya wanawake hawapo pamoja nao katika maadhimisho hayo ya siku ya wanawake kutokana na kushambuliwa na kuuawa na wengine wanahofia usalama wao.

Hotuba yake hiyo mbele ya Bunge la kitaifa ,ilizungumzia kwa kina Jukumu la wanawake katika kutafuta amani ya Afrika ya Kati na kuongeza kuwa hawataendelea kuhamasisha kutokuvumiliana na chuki miongoni mwa ndugu zao waislamu na wakristo ambao wamekuwa wakiishi pamoja kwa amani.

Usalama katika mji mkuu wa Bangui unazorota hatua kwa hatua na kwa kiasi alisema Panza, na kulaumu fitna zinazopenyezwa kwa vijana wa nchi hiyo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.