Pata taarifa kuu
RWANDA-DRC-Mazungumzo

Kundi la waasi wa Rwanda la FDLR liko tayari kwa mazungumzo na Serikali ya Rwanda

Waasi wa Rwanda wa FDLR wanapiga vita utawala wa Paul Kagame ambao wanapiga kambi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametangaza kwa mara nyingine tena wako tayari kujisalimisha pamoja na silaha zao kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kwa ajili ya mazungumzo na serikali ya Rwanda. Kundi la FDLR limekua likiomba mara kadhaa mazungumzo na serikali ya Rwanda bila hata hivo mafanikio.

Wapiganaji wa kundi la FDLR katika kijiji cha Lushebere, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, novemba 2008.
Wapiganaji wa kundi la FDLR katika kijiji cha Lushebere, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, novemba 2008. AFP PHOTO/ Tony KARUMBA
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa mwaka uliopita, waasi hao walionyesha nia yao ya kusalimisha silaha zao kwa sharti la kuzungumza na utawala wa Paul Kagame wa Rwanda, jambo ambalo mara kadhaa serikali ya Kigali imetupilia mbali kwa kuwahusisha na tuhuma za mauwaji ya kimbari wanaodaiwa kutekeleza waasi hao.

Kundi la FDLR limekua likiukosoa utawala wa Paul Kagame, na kukanusha tuhuma za serikali ya Kigali dhidi yake kwamba linahusika katika mauwaji ya halaiki yaliyotokea Rwanda mwaka 1994.

Kundi hilo linabaini kwamba kuhusishwa kwao katika mauwaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda, ni mbinu za utawala wa Paul Kagame ili aendeleye kusalia madarakani, bila hata hivyo kuzingatia kua Rwanda ni taifa la wananchi wote wa Rwanda, limeendelea kufahamisha kundi hilo la FDLR.

Hivi karibuni waziri mkuu wa zamani wa Rwanda Faustin Twagiramungu, alifahamisha kwamba chama chake kimejiuga na kundi la FDLR.

Serikali ya Rwanda inalichukulia kundi la FDLR kwamba linaundwa na wanamgambo wa kihutu (Interahamwe) kutoka chama cha zamani cha MRND cha hayati rais wa zamani wa Rwanda, Juvenal Habyarimana.

Serikali ya DRC imeelezea hatua hiyo kuwa jambo la kutia moyo pamoja na kuwatahadharisha waasi hao wazingatie taratibu zote za kimataifa kwa ajili ya kuandaliwa kurejea makwao kwa msaada wa MONUSCO.

Waziri wa Mawasiliano akiwa pia msemaji wa serikali ya Jamhuru ya Kidemokrasia ya Congo, Lambert Mende, amepongeza hatua hio.

β€œKwa vyovyote hivyo ni jambo jema ili mradi lithibitishwe, na ni njia bora kumaliza umwagaji damu. Hayo mengine yanahusu nchi yao kwa msaada wa umoja wa mataifa hususan shirika la kuhudumia wakimbizi, hadi watuthibitishie kwamba kwa upande wao wamesitisha uasi huo, amesema Mende, huku akibaini kwamba wale watajisalimisha pamoja na silaha zao watapewa ulinzi wa serikali ya DRC na Jumuiya ya Kimataifa.

Katika hatuwa nyingine, Shirika la kutetea haki za kisheria nchini DRC ACAJ limetangaza orodha ya watu 70 ambao wako kizuizini kwa sababu za kisiasa na kuomba waachiwe huru kwa mujibu wa msamaha wa rais unaosubiriwa kwa vile wao ni wapinzani ambao wanapambana bila vurugu na silaha.
Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.