Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM

Kiongozi wa Boko Haram akiri kuhusika na shambulizi katika mitambo ya jeshi la Nigeria

Kiongozi wa kundi la kigaidi la Boko Haram la nchini Nigeria amekiri kundi hilo kuvamia eneo la mitambo ya kijeshi iliyoko mji wa Kaskazini mwa nchi hiyo, Maiduguri mapema mwezi huu. Shirika la habari la Ufaransa AFP limebainisha taarifa hiyo baada ya kuipata video ya dakika 40 inayomuonesha kiongozi wa kundi hilo Aboubakar Shekau akimshukuru Mungu kwa kuwapatia ushindi katika shambulizi hilo.

REUTERS/IntelCenter/Handout
Matangazo ya kibiashara

Video hiyo inamuonesha Shekau akizungumza kwa lugha ya Kiarabu, Kihausa na Kanuri ambazo huzungumzwa Kaskazini mwa Nigeria anasikika akidai kushambulia mji huo na kuwazidi nguvu wanajeshi wa serikali.

Katika shambulizi hilo jeshi lilisema wanajeshi wake wawili waliuawa na wapiganaji 24 waliuawa, lakini Shekau amesema wapiganaji wake saba tu ndio waliuawa katika shambulizi la bomu na kurushiana risasi.

Jeshi la Nigeria lililazimika kutangaza amri ya kutotoka nje kwa saa 24 mjini Maiduguri katika kipindi cha mashambulizi hayo ambapo wananchi wawili waliripotiwa kuuawa katika shambulizi hilo.

Mwezi uliopita Marekani ililitangaza kundi la Boko Haram na lile la Ansaru yote ya nchini Nigeria kama makundi ya kigaidi yanayotishia usalama wa dunia.

Maelfu ya watu wamepoteza maisha nchini Nigeria toka kuanza kwa harakati za kundi la Boko Haram mwaka 2009.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.