Pata taarifa kuu
DRCongo-AU

Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika AU, Nkosazana Dlamine Zuma azuru jijini Kinshasa mwishoni mwa juma

Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika AU Nkosazana Dlamine Zuma anataraji kufanya ziara mwishoni mwa juma hili nchini jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo katika mpango wa kuchcochea uwiano wa mashariki ya nchi hiyo.

Nkosazana Dlamine Zuma, rais wa kamisheni ya Umoja wa Afrika AU
Nkosazana Dlamine Zuma, rais wa kamisheni ya Umoja wa Afrika AU
Matangazo ya kibiashara

Nkosazane Dlamini Zuma anafanya ziara hiyo chini ya mualiko wa serikali ya rais Joseph Kabila kuanzia Octoba 20 hadi 22.

ziara hiyo ya kwanza ya kiongozi huyo wa juu wa Umoja wa Afrika, inakuja kufuatia makubaliano yaliofikiwa jijini Addis Abeba nchini Ethiopia, Februari 24 mwaka 2013 chini ya viongozi 11 wa mkutano wa viongozi wa nchi za ukanda wa maziwa makuu.

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, DRCongo inatakiw akufanya mageuzi ya ndani kuhusu idara za usalama na mabadiliko ya kisiasa, hususan swala linalo zua utata la kutowa madaraka zaid kwa mikoa.

Aidha nchi nyingi kumi zilizo saini mkataba huo, zilijikubalisha kutovumilia na kutotowa msaada wa aina yoyote kwa makundi yanayo yumbisha usalama wa taifa hilo tangu miongo miwili.

Mataifa ya Rwanda na Uganda majirani ya DRCongo ni miongoni mwa mataifa yaliosaini mkataba huo. Umoja wa Mataifa unayatuhumu mara kadhaa mataifa hayo kutowa msaada kwa kundi la waasi wa M23 wanaopambana na majeshi ya serikali ya taifa hilo ya FARDC tangu mwezi Mei mwaka 2012 katika mji wenye utajiri wa madini wa kivu ya Kaksazini, tuhuma ambazo srikali ya Kigali na Kampala zinatupilia mbali.

Katika ziara hiyo bibi Dlamine Zuma atakutana na viongozi wa juu wa serikali ya Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, mwenyekiti wa baraza la seneti, spika wa bunge, wawakilish wa nchi mbalimbali za Afrika nchini humo, pamoja na wanadiplomasia wa nchi wanachama wa baraza la Uslama la Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.