Pata taarifa kuu
Afrika ya Kati- Usalama

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius atangaza kuongeza wanajeshi zaidi nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati

Serikali ya Ufaransa imeahidi kuongeza wanajeshi wake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa ajili ya ulinzi wa usalama wakati huu taifa hilo likakabiliwa na hali ya vurugu huku kiongozi wa serikali ya mpito, Mitechl Djotodia akitakiwa kutekeleza ahadi yake ya kuandaa uchaguzi huru uliopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka 2015.

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius akiwa kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius akiwa kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa REUTERS/Keith Bedford
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza akiwa ziarani nchini humo, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius amesisitiza kampeni ya nchi yake kuhusu suala la usalama kwenye nchi hiyo, kampeni ambayo inaungwa mkono na Umoja wa Ulaya EU.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa, Laurent Fabius amezitaka nchi wanachama wa ECOWAS kuhakikisha zinashirikiana katika kuimarisha usalama kwenye ukanda wa Afrika Magharibi dhidi ya makundi ya uasi ambayo yanahatarisha usalama kwenye nchi zao.

Waziri huyo wa Ufaransa wa mambo ya nje ambaye alifanya ziara fupi nchini humo amesema licha ya kuwa ziara hiyo ilikuwa ya muda mdogo, imekuja kuonyesha uungwaji mkono wa serikali yake katika kutafuta suluhu ya matatizo yaliopo nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Akiwa katika Ikulu ya taifa nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Laurent Fabiusamekutana ana kwa ana na kiongozi wa taifa hilo rais Michel Djotodia pamoja na kiongozi wa baraza la kipindi cha mpito Alexandre- Ferdinand N'Guendet pamoja na waziri mkuu Nicolas Tiangaye.

ujumbe wa waziri huyo kwa viongozi wa Afrika ya Kati ulikuwa ni kuwataka wahakikishe usalama unarejea, kuboresha hali ya kibinadamu katika nchi hiyo na kuandaa chaguzi zijazo.

Uchaguzi ambao Laurent Fabius anatarajikuwa utafanyika mwishoni mwa mwaka 2015 na ambapo viongozi wa kipindi cha mpito hawatoshiriki katika chaguzi hizo.

Kiongozi huyo wa maswala ya Diplomasia nchini Ufaransa ametsngaza kuwa serikali yake itawatuma wanajeshi zaidi kabla ya mwishoni mwaka huu kumalizika.

Mbali na viongozi hao, Laurent Fabius amekutana pia na na viongozi wa kidini nchini humo na kuwapa ujumbe wa Umoja wa Ulaya ambao unawataka kuhakikisha taifa hilo halitumbukii katika machafuko ya kidini wananchi wa taifa hilo wamekuwa wakieshi pamoja katika mshikamano haitovumilika kuona wanashambuliana kutokana na tofauti zao za kidini.

Kabla ya kutamatisha ziara yake hiyo nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Laurent Fabius amezuru Hospitali wanakolazwa watoto ambao kwa sehemu kubwa walioathirika kutokana na machafuko yanayoendelea nchini humo.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.