Pata taarifa kuu
ICC-LIBYA

ICC yasema Mkuu wa zamani wa Inteljensia nchini Libya Abdullah al-Senussi anaweza kushtakiwa nyumbani

Mahakama ya Kimataifa ya ICC imeamua kuwa aliyekuwa Mkuu wa Inteljensia nchini Libya wakati wa uongozi wa Marehemu Muamar Kadhafi, Abdullah al-Senussi sasa anaweza kufunguliwa mashtaka nchini mwake.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya ICC inaamanisha kuwa haitamtaka tena Senussi kufika Hague na kumfunguliwa Mashtaka ya mauaji  ya raia yanayomkabili  wakati wa mapambano kati ya majeshi ya serikali na waasi.

Mwaka 2011 Mahakama hiyo ilitoa hati ya kukamatwa na kufikishwa Hague kiongozi huyo wa zamani wa kitengo cha inteljensia nchini Libya baada ya kutoroka katika nchi yake.

Serikali ya Mauritania ilimkamata Sennusi na kumrudisha nchini Libya mwaka uliopita baada ya serikali ya mpito kipindi hicho kusema kuwa ilikuwa na uwezo wa kumfungulia mashtaka.

Hata hivyo, ICC imesema kuwa umauzi huo haushirikiani kwa vyovyote vile na kesi inayomkabili mwanaye Gaddafi , Saif al-Islam Gaddafi ambaye anatakiwa katika Mahakama hiyo ya Kimataifa ili kufunguliwa Mashtaka.

ICC inaitaka serikali ya Libya kumsafirisha Saif al-Islam Gaddafi mjini Hague kwa kile wanachosema kuwa katika Mahakama hiyo atapata haki lakini Serikali ya Libya inasisitiza kuwa ina uwezo wa kuhakikisha kuwa haki inatendeka.

Saif Gaddafi kwa sasa anashikiliwa katika mji wa Zintan Magharibi kwa nchi hiyo na wiki iliyopita waasi wanaomzuia walikataa kumfikisha Mahakamani jijini Tripoli wakati kesi ya Senussi ilipoanza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.