Pata taarifa kuu
SUDAN

Sudan na Sudan Kusini zamaliza mvutano mafuta, Sudan kuamua kura ya maoni Abyei

Sudan na Sudan Kusini zimeahidi kutekeleza makubaliano yao ya kiuchumi na usalama ili kuendeleza usafirishaji wa mafuta uliositishwa baada ya Khartoum kuishutumu Juba kuwaunga mkono waasi.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano wa viongozi wa Mataifa hayo, Rais Omar al-Bashir amesema mafuta toka Sudan Kusini yataendelea kusafirishwa kupitia Sudan baada ya makubaliano ya kuondoa tofauti zao kufanikiwa.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir anasema huu ni wakati muafaka kwa pande zote kuhakikisha wanatekeleza makubaliano yao kwa muda uliopangwa.

Sudan na Sudan Kusini pia zimekubaliana kuruhusu watu wa pande zote kuvuka mipaka yao bila vikwazo na hata kufanya biashra.

Wakati huohuo waakuu wa Sudan wanasema kuwa hivi karibuni watatangaza rasmi ikiwa mwezi ujao watashiriki kwenye kura ya maoni kuamua kama jimbo la Abyei lenye utajiri wa mafuta liko Kusini ama kaskazini.

Suala la Abyei, linakuja wakati ambapo Rais Omar Hassan Ahmed El Bashir wa Sudan na mwenzake wa Kusini, wamemaliza mkutano muhimu mjini Khartoum ambako waliamua kuwa mabomba ya mafuta yataendelea kutiririka na wala hayatafungwa kama ilivyohofiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.