Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Kipindi cha mpito kuanza leo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya kuapishwa kwa Michel Djotodia

Michel Djotodia, kiongozi ambaye alichukua madaraka katika nchini jamuhiri ya Afrika ya kati Machi 24, anakula kiapo le Jumapili mbele ya Mahakama ya KiKatiba kama rais wa sita wa nchi, hiyo na kuanza rasmi kipindi cha mpito cha miezi 18 kitacho kamilika kwa kufanya uchaguzi mkuu katika nchi hiyo iliotumbukia katika vurugu tangu kuangushwa kwa utawala wa François Bozizé.

Michel Djotodia
Michel Djotodia
Matangazo ya kibiashara

Orodha ya mambo yatayo pewa kipaumbele ni mengi. Lakini uharaka zaidi ni kurejesha amani na usalama vilivyo toweka katika nchi hiyo. Pamoja pia na kuboresha uongozi, na kufufua uchumi uliotetereka tangu miongo kadhaa.

Katika kurejesha amani na usalama, rais Michel Djotodia amepanga kuwapokonya silaha wale wote wanaozimiliki kinyume cha sheria na kuwarejesha wapiganaji zamani katika maisha ya kiraia.

Wakati rais huyo akijiandaa kula kiapo, Francois Bozize aliepinduliwa madarakani ameukosoa ushiriki wa Chad na Sudan kuingilia Kati maswala ya ndani mwa taifa hilo tangu kuanguka kwa utawala wake mwezi Machi. Msemaji wake, Lawi Yakété, amekemea uwepo wa Rais Idriss Deby wa Chad katika sherehe zinazo tarajiw akuwepo leo jijini Bangui.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.