Pata taarifa kuu
LIBYA

Waziri mkuu wa Libya kulisuka upya Baraza la Mawaziri na taasisi ya usalama wa ndani

Waziri mkuu wa Libya Ali Zeidan, ameahidi kuwa kufanya mabadiliko katika taasisi ya usalama wa ndani sambamba na baraza la mawaziri ikiwa ni jitihada za kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa na kumaliza ghasia zinazoendelea kushuhudiwa nchini humo.

Reuters / Zitouny
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huo umekuja siku moja baada ya kutokea kwa mashambulizi mawili nje ya mahakama mjini Banghazi ambapo watu watu zaidi ya arobaini walijeruhiwa.

Zeidan amesema mabadiliko katika shirika la usalama wa ndani ambalo kwa kiasi kikubwa lilisaidia kumuweka madarakani Rais wa zamani wa Taifa hilo marehemu Kanali Muammar Gaddafi, yatasaidia kupambana na changamoto zinazoikabili Libya kwa sasa kama vile mashambulizi ya mabomu na mauaji hasa katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo.

Libya haijawa na Waziri wa ulinzi tangu tangu mwishoni mwa mwezi june baada ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo kwa aliyekuwa waziri wa ulinzi Mohammed al-Barghathi.

Tayari Waziri mpya wa ulinzi ameishateuliwa na siku ya jumatano Waziri Mkuu Zeidan anatarajia kuwasilisha orodha ya Mawaziri wapya mbele ya mamlaka za nchi hiyo.

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya EU Catherine Ashton ameeleza kusikitishwa na mashambulizi yanayojitokeza nchini Libya na ametaka wahusika wasakwe na kufikiswhwa kwenye vyombo vya sheria.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.