Pata taarifa kuu
MALI

Wagombea Urais nchini Mali waorodheshwa siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu

Orodha ya majina 26 ya wagombea urais nchini Mali imewekwa hadharani siku ya ijumaa, Haider Aichata Cisse ni mwanamke pekee aliyeingia katika kinyang'anyiro hicho miongoni mwa wagombea walioorodheshwa.

REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Baadhi ya majina yaliyomo kwenye orodha hiyo ni pamoja na Ibrahim Boubacar Keita, Cheick Modibo Diarra, Modibo Sidibe na Soumana Sacko, wote hao ni wanasiasa waliowahi kushika nyadhifa za Uwaziri Mkuu wa Mali.

Kwa mujibu wa taarifa ya mahakama majina nane likiwamo moja wa mwanamke yaliwekwa kando baada ya wahusika kushinda kukamilisha masharti ya udhamini.

Huenda kukawa na duru la pili kati ya vinara wawili wataoshika nafasi ya juu endapo hakutakuwa na mgombea akakayepata kura nyingi zaidi katika duru la kwanza.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu na kama hatapatikana mshindi aliyepita kwa kura nyingi zaidi kutakuwa na duru la pili tarehe 11 ya mwezi Agosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.