Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Serikali mpya yatangazwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Nicolas Tiangaye hatimaye ametangaza serikali mpya na kutaja baraza la Mawaziri 34 huku nyadhifa muhimu zikipewa kwa waasi wa Seleka.

Matangazo ya kibiashara

Wizara tisa zimekabidhiwa kwa viongozi  hao wa Seleka waliongoza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya rais Francois Bozize jijini Bangui ambaye alikimbilia ukimbizoni  mapema mwaka huu.

Viongozi wa Mashirika ya kiraia nchini hiumo yamepewa nyadhifa 16 huku nyadhifa zinazosalia zikiwaendea wanasiasa mbalimbali.

Rais Michel Djotodia aliyejitangaza rais wa nchi hiyo baada ya kufanikisha mapinduzi ya kijeshi nchini humo ni Waziri wa Ulinzi nchini humo na alimteua Tiangaye kuwa Waziri Mkuu kuongoza serikali.

Djotodia anaongoza nchi hiyo kwa kipindi cha mpito kwa miezi 18 ijayo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu nchini humo kulingana na mazungumzo ya Libreville nchini Gabon baada ya mapinduzi ya kijeshi jijini Bangui.

Miongoni mwa wanachama wa Seleka waliopewa nyadhifa za Mawaziri ni pamoja na Gontran Djono atakayehusika na madini, Nourendine Adam wa usalama huku Christophe Gazam Betty akitajwa Waziri mpya wa habari na Mawasiliano.

Makubaliano ya Libreville iliyofanyika mwezi Aprili kuwajumuisha wawakilishi wote kutoka ndani ya serikali hiyo.

Serikali mpya ya Waziri Mkuu Tiangaye ina jukumu la kuimarisha usalama nchini humo hasa jijini Bangui na kuimarisha uchumi wa taifa hilo ambao umeonekana kudorora tangu kuanguka kwa serikali ya Bozize.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.