Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Jamhuri ya Afrika ya Kati yaomba kusaidiwa baada ya kutengwa na Umoja wa Afrika

Serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati inayoongozwa na Waziri Mkuu Nicolas Tiangaye imeanza kuomba huruma kutoka Jumuiya ya Kimataifa ili iweze kusaidiwa kutokana na kutengwa na Mataifa mengi ya Afrika tangu yafanyike mapinduzi.

AFP PHOTO/JOHN THYS
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Tiangaye anatarajiwa kufanya safari kuzuru mataifa ya Ulaya ili kuhakikisha anazishawishi nchi hizo kuisaidia kwa hali na mali pamoja na uongozi ulio chini ya Muungano wa Seleka.

Hatua hiyo imeungwa mkono na Mjumbe Maalum wa Masuala ya Francophonie nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Louis Michel ambaye amesema huu ni wakati muafaka wa kuisaidia serikali hiyo ya Bangui.

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika ya Kati ECCAS walitangaza kuitambua serikali ya mpito ya Rais Michel Djotodia ya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ingawa bado wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Francois Bozize wameendelea kutoa wito kwa Umoja wa Afrika AU na Jumuiya ya Kimataifa kutoitambua serikali hiyo.

Umoja wa Afrika AU umeendelea na msimamo wake wa kutoitambua serikali hiyo ya Muungano wa Seleka ambayo imeingia madarakani kwa nguvu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.