Pata taarifa kuu
Cameroon

Raia saba wa Ufaransa waliotekwa nyara nchini Cameroon waachiliwa huru

Familia ya watu saba raia wa Ufaransa waliotekwa nyara na waasi wa Kislamu miezi miwili iliyopita nchini Cameroon wameachiliwa huru.

Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya rais wa Ufaransa imesema kuwa familia hiyo iko katika afya nzuri na Waziri wa Mambo ya nje Laurent Fabius anaelekea nchini Cameroon kuiona familia hiyo.

Rais  wa Cameroon Paul Biya naye amethibitisha kuachiliwa huru kwa familia hiyo kutoka Ufaransa ambayo ilitekwa nyara na kuwasafirisha nchini Nigeria.

Familia hiyo kwa sasa imepata hifadhi katika Ubalozi wa Ufaransa jijini Yaounde nchini humo ikisubiri kurejea nyumbani.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa serikali yake haikulipa kikombozi kwa waasi hao wa Kislamu waliowateka nyara raia hao wa Ufaransa.

Familia ya raia hao wa Ufaransa walikuwa wanaishi nchini Cameroon tangu mwaka 2011 na walitekwa nyara na kundi la Kiislamu walipokuwa wamekwenda kutalii katika mbuga ya kitaifa ya Waza.

Kundi la Boko Haram kutoka nchini Nigeria limekuwa likishukiwa kutekeleza utekwaji nyara huo na kuwaficha raia hao wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.