Pata taarifa kuu
TUNISIA

Rais wa Tunisia Moncef Marzouki asema chama chake kitasalia serikalini

Rais wa Tunisia Moncef Marzouki ametangaza kuwa chama chake kisichoegemea udini kitasalia katika serikali ya muungano nchini humo,  lakini anataka kujiuzulu kwa Mawaziri wa mrengo wa  Kiislamu ili kuepuka vurugu za kisiasa nchini humo.

Le président tunisien Moncef Marzouki, le 6 février 2013.
Le président tunisien Moncef Marzouki, le 6 février 2013.
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, chama hicho cha CPR  kimetishia kujiondoa katika serikali hiyo ikiwa hakutakuwa na  mabadiliko katika serikali hiyo kwa kipindi cha wiki moja ijayo.

Chama cha rais Marzouki kinataka kujiuzulu kwa  Mawaziri wa Mambo ya ndani, Sheria na yule wa nchi za kigeni kutoka kwa chama cha Waziri Mkuu Hamadi Jebali cha Ennahda.

Siku mbili zilizopita, chama cha rais Marzouki CPR kiliwasilisha orodha ya Mawaziri wake kujiuzulu lakini matakwa yao yakaridhiwa na chama cha Ennahda.

Chama cha CPR pia kinapinga mpango wa Waziri Mkuu Jebali wa kuunda serikali isiyowajumuisha wanasiasa kwa kile inachosema itawarejesha madarakani washirika wa karibu wa rais wa zamani Zine El Abidine Ben Ali.

Pendekezo la Waziri Mkuu Jebali pia limepingwa na chama cha Ennahda kwa kile inachosema kitasababisha vurugu za kisiasa nchini humo ambacho pia linatuhumiwa kusababisha kifo cha kiongozi wa upinzani Chokri Belaid.

Kifo cha kiongozi huyo kilisababisha machafuko makubwa nchini humo huku waandamanaji wakishinikiza kujiuzulu kwa viongozi wa serikali nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.