Pata taarifa kuu
NIGERIA

Wahudumu wa chanjo ya ugonjwa wa polio wauawa nchini Nigeria

Watu wenye silaha wamewaua wahudumu kumi waliokuwa wakitoa chanjo ya ugonjwa wa polio ijumaa nchini Nigeria kwa lengo la kupinga utoaji wa chanjo hiyo kwa jamii hiyo. Kwa mujibu wa taarifa toka nchini humo waliouawa ni wanawake tisa pamoja na mwanaume mmoja ambao walikutwa katika vituo viwili tofauti katika jimbo la kaskazini la Kano.

guardian.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Raisi wa Nigeria Goodluck Jonathan amelaani vikali mauaji ya watoa huduma hao tukio ambalo limezuka baada ya serikali kuanzisha kampeni maalumu ya kupambana na ugonjwa wa polio.

Umoja wa mataifa UN na serikali ya Marekani zimelaani mauaji hayo kupitia taasisi ya afya ya kimataifa na kusema kuwa kupinga utoaji wa chanjo hiyo ni kukandamiza mpango wa msingi wa kuokoa maisha.

Msemaji wa serikali ya marekani Victoria Nuland alinukuliwa akionya juu ya vitendo vyovyote vitakavyohatarisha utoaji wa chanjo hiyo havitavumiliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.