Pata taarifa kuu
SOMALIA-UFARANSA

Kundi la Al Shabab latangaza kuwa limemuaa ofisa wa kijajusi wa Ufaransa Denis Allex

Kundi la kigaidi la Al-Shabab nchini Somalia linasema limemuua Denis Allex ofisaa wa ujasusi raia wa Ufaransa ambaye amekuwa akizuiliwa kama mateka kuanzia mwaka 2009.Licha ya kundi la Al-Shabab kutangaza kuwa tayari limemuua Denis Allex serikali ya Ufaransa inasema inaamini kuwa ofisa wake aliuawa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa juhudi za kumwokoa.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Awali Al-Shabab ilikuwa imetishia kumuua Allex kwa kile walichokisema kuwa serikali ya ufaransa ilikuwa imekataa kuzungumza nao ili kumwachilia mateka huyo.
 

Aidha, Al Shabab imeeleza kuwa hatua ya Ufaransa kuanza kuwashambulia waasi wa Kiislamu Kaskazini mwa Mali imechangia wao kuchukua hatua ya kumuua ofisa huyo wa Ujasusi.

Ijumaa iliyopita Makomandoo wa Ufaransa wapatao 50 waliwashambulia wanamgambo wa Al-Shabab katika ngome yao ya Bulo Mare kujaribu kumwokoa bwana Alex lakini oparesheni hiyo ikagonga mwamba na kusababisha vifo vya wanajeshi wawili wa Ufaransa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.