Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Utekelezaji wa makubaliano baina ya Waasi wa Seleka na Jamhuri ya Afrika ya Kati waanza rasmi

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize amemvua madaraka Waziri Mkuu wa serikali yake Faustin Archange Touadera ikiwa ni mojawapo ya hatua za utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali na waasi wa Seleka katika mazungumzo ya kusaka amani ya Taifa hilo yaliyofanyika mjini Libreville nchini Gabon.

REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la kuvuliwa madaraka kwa Waziri Mkuu lilitolewa kupitia radio ya umma jana jumamosi na nafasi hiyo inatarajiwa kuzibwa na Waasi wa Seleka ambao wamekubaliana kuunda serikali ya umoja wa Kitaifa na serikali iliyopo madarakani hivi sasa.

Uamuzi huo umepokelewa kwa furaha na wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao wameathiriwa na mapigano hayo yaliyoambatana na ukikwaji mkubwa wa haki za binadamu hususani wanawake na watoto.

Vyanzo vya habari toka upande wa upinzani vimedokeza kuwa huenda nafasi hiyo ikachukuliwa na Mwanasheria Nicolas Tiangaye ambaye aliongoza ujumbe wa waasi katika mazungumzo ya nchini Gabon, wakati wengine wakimtaja mwanasheria mwingine Henri Pouzere ambaye naye ameshiriki katika mchakato huo.

Mazungumzo ya amani yaliyofikia uamuzi huo yandaliwa na Jumuia ya Kiuchumi ya nchi za Afrika ya Kati yalihudhuriwa na Rais wa Gabon Ali Bongo, Rais wa Jamuhuri ya Congo Brazaville Denis Assou Nguesso ambaye pia ni msuluhishi wa Mgogoro huo na Rais wa Chad Idriss Deby Itno ambaye ni Mshirika wa karibu wa Bozize.

Wanajeshi takribani mia tano kutoka Gabon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Chad na Cameroon walipelekwa nchini humo kulinda amani mwaka 2008, na kumekuwa na taarifa kuwa wameanza kuondoka nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.