Pata taarifa kuu
Gabon

Mzungumzo ya Amani yaendelea leo Kati ya Serikali ya Bozize na Waasi wa Seleka.

Mazungumzo ya Amani ya kumaliza Uasi nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati yanatarajiwa kuendelea hii leo huku kukiwa hakuna makubaliano yeyote baada ya Waasi kutaka kujiuzulu kwa Rais wa Taifa hili Froncois Bozize na kufikishwa katika Mahakama ya kimataifa ya Uhalifu wa kivita, ICC. 

Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Froncois Bozize
Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Froncois Bozize REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Waasi wa Seleka waliwasilisha shinikizo lao kwa maandishi ujumbe uliosambambazwa siku ya kwanza ya mazungumzo.

Waasi hao wanamshutumu Rais Bozize kwa kile walichodai ana makosa ya uhalifu wa kivita na Uhalifu dhidi ya Ubinaadam yakiwemo kukamata na kushikilia watu bila utaratibu na kuwafunga watu pasipo na makosa, vitendo vya utekaji nyara, kuwateka watu na kuwapeleka kusikojulikana na mauaji.

Mazungumzo yanayohusisha pande tatu kati ya Waasi, Serikali ya Jamuhuri ya Afrika ya Kati na Vyama vya Upinzani yanasimamiwa na Jumuia ya Kiuchumi ya nchi za Afrika ya kati, mjini Libreville nchini Gabon.
 

Mzungumzo haya yalilenga kujadili juu ya makubaliano ya amani yaliyotiwa saini kati ya mwaka 2007 na 2011 ambapo waasi wamedai kukiukwa kwa Makubaliano hayo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.